Mzimu wa Posho Bunge la Katiba Waibuka Tena, Kamati ya Uandishi Wataka Posho ya Sh500,000 Kwa Siku

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mzimu wa posho umeibuka upya katika Bunge la Katiba, safari hii wajumbe wake wa Kamati ya Uandishi wakiomba walipwe posho maalumu ya Sh500,000 kwa siku kutokana na kazi ya kuandika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge zinasema kuwa tayari maoni ya wajumbe yamewasilishwa kwa uongozi kwa ajili ya uamuzi.

Wajumbe wa kamati hiyo kwa sasa wanalipwa posho maalumu ya Sh210,000 zaidi kwa siku, nje ya ile ya Sh300,000 kwa siku wanayolipwa wajumbe wote wa Bunge hilo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi-CCM inahusisha baadhi ya vigogo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Vigogo hao ni pamoja Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro, Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman aliyejiuzulu ujumbe wa kamati hiyo hivi karibuni kwa sababu ambazo hazijaelezwa.

Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad pamoja na kukiri kuwa kamati hiyo imeomba kuongezwa kiasi hicho cha posho, alisema Kamati ya Uongozi ambayo ndiyo huamua, haijayajadili maombi hayo na kuyatolea uamuzi.

Chenge hakupatikana jana kuzungumzia maombi hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mshindweeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahaha,Na walegeeeeeeeeeeeee!

      Delete
  2. nawakakamaeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Tutawashushia nyuki mshindwe kukaa.

    ReplyDelete
  4. Hebu kuweni na uchungu na Wananchi wenu,hela zote hizo jamani?
    Au mnadhani hazina mnayoiweka hapa duniani mtakufa nayo?
    kuna watu wanakosa hata hela ya matibabu nyie mnajilimbikizia mahela kiasi hicho?
    JAMANI HAMTAZIKWA NAZO.

    ReplyDelete
  5. Mxiuuuuuuuuu,yani hapa cna hata cha kucomment as nimeshikwa na mshangao,hivi hawa ni watanzania wenzetu au wahamiaji,duuuu yn hawana hata huruma??mxiuuuuuu! Washindwe na wasisikilizwe kabisa hayo maombi yao!

    ReplyDelete

Top Post Ad