Ebola Tena Marekani ..Daktari Aliyekuwa Akimtibu Yule Mgonjwa wa Ebola Aliyefariki nae Akutwa na Virusi Hivyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mfanyakazi aliyemtibu mgonjwa wa Ebola Thomas Eric Duncan nchini Marekani kabla hajafariki ameripotiwa kukutwa na virusi vya Ebola kutokana na utafiti wa afya aliofanyiwa ambapo kwa sasa amewekwa kwenye kitengo maalumu huku ikisemekana pamoja na kuvaa mavazi ya kumkinga kuambukizwa virusi, haikusaidia chochote.

Duncan ambaye alipata virusi hivyo vya Ebola alipokuwa mjini Liberia alifariki Jumatano ambapo mlipuko huu wa virusi vya Ebola kutoka nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone imethibitishwa kuwa na waathirika 8300 na vifo vya kukaribia 4033.
Hospitali imethibitisha kuwa njia za kujikinga na maambukizi hayo ya Ebola zinafatwa kwa uangalizi mkubwa na wafanyakazi wote ambao wanafanya kwenye kituo hicho cha afya cha Texas Health Presbyterian ambapo mkuu wa kituo hicho Dr. Tom Frieden amesema kuna uwezekano mfanyakazi huyo hakufata njia zote husika za kujikinga na ugonjwa huo.
Mkuu wa kituo hicho cha afya alikiambia chombo cha habari cha Marekani CBS kwamba watafanya uchunguzi ili kujua ni jinsi gani muhudumu huyo wa afya alipata virusi hivyo vya Ebola na kwamba wote ambao walimuhudumia Duncan watafanyiwa uchunguzi ili kujua kama na wao wamepata virusi hivyo vya Ebola.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kama marekan wanapata maambukizi pamoja na uwezo wao mkubwa. Watanzania tumuombe sana Mungu mwenyewe atuepushe kabisa na maambukizi kuingia nchini kwetu.

    ReplyDelete

Top Post Ad