Amini, Usiamini, Maazimio yaliyotokana na Maridhiano ni Makali kupita Maazimio ya Mwanzo ya PAC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ukiangalia kwa makini maazimio ya kuwawajibisha viongozi wa umma walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika sakata hili la Tegeta Escrow, utaona kwamba maazimio yaliyotokana na maridhiano kati ya CCM na wapinzani ni makali kupita maazimio ya mwanzo ya PAC.....


Maazimio ya mwanzo ya PAC pamoja na mambo mengine yalipendekeza kuwawajibisha wafuatao : wziri wa nishati na madini, naibu wake pamoja na katibu wa wizara hiyo ikiwa ni pamoja na wazri mkuu...


Pamoja na kwamba Waziri mkuu hajawajibika katika maazimio yaliyotokana na maridhiano, hao wengine wote (ukimwondoa Naibu waziri ambaye hata hivyo hakuhusika moja kwa moja), bunge limependekeza wawajibishwe na kuongeza idadi ya watu wengine wa kuwajibika ambao ni pamoja na waziri wa ardhi (Tibaijuka) na wenyeviti watatu wa kamati za kudumu za bunge...


Kwa kweli nimshukuru sana Mbowe kwa uamuzi aliouchukua dakika za mwisho wa kutishia kususia bunge kitu ambacho kimepelekea haya yote kutokea. Katika hali ya kawaida na kwa jinsi lile Bunge lilivyokuwa linaendelea, mapendekezo dhaifu yalishakuwa yamepitishwa kuhusiana na Maswi na ndio hayo hayo yaliyokuwa yanaelekea kupitishwa kwa Muhongo na Werema....Waziri mkuu obvious ange-sevu kwani trend ndivyo ilivyokuwa inaenda......The best we could get at that time ilikuwa mapendekezo ya kuwajibishwa kwa Werema na Muhongo ambapo hata hivyo CCM walikuwa karibu kushinda vita hivyo kama walivyokuwa wameshinda kwa Maswi......


Mimi binafsi (naamini hata watu wengine wengi tu) niliona hakuna kinachoweza kufanyika zaidi ya Muhongo na Werema kupata mapendekezo kama yaliyotolewa kwa Maswi !. Ungewezaje kuwa na mapendekezo tofauti dhidi ya Muhongo na Werema katika mazingira yale ambapo tayari umeshapitisha mapendekezo tofauti kwa Maswi ? Ndio maana Zitto (hata Mdee kama uliangalia vizuri - alionyesha kwa ishara) akasuggest mapendekezo hayo hayo yatumike kwa waliobaki kwa sababu hiyo ilikuwa issue ya common sense tu ! Pinda, Werema, Muhongo, Maswi wote ni wateule wa Rais.....sasa kama umeamua Maswi apelekwe kwa Rais kwa hatua yeyote ile, sioni sense ya kuamua vinginevyo kwa hao wengine......Mimi binafsi niliona alichokipendekeza Zitto kilikuwa sahihi !


CCM nao (sijui ilikuwa malicious au genuine), walitengeneza mazingira mazuri sana ya majadiliano kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuibuka na kupinga utaratibu wote na kutishia kususa kama alivyofanya Mbowe. Binadamu ni binadamu tu, mkiwa mmekaa katika mazingira ya kuelewana na kuongea kiistaarabu na kujadiliana na kukubaliana baadhi ya mambo katika spirit hiyo na ikafika mahali kukawa na ugumu kidogo huwa inatokea tu natural mnajaribu ku-compromise....it is very natural. Na ndio maana katika mazingira yale ilikuwa rahisi kukubali mapendekezo ya Chenge ambayo yalionekana ku-accomodate position ya CCM na ya wapinzani kwa kiasi cha kutosha ukilinganisha na mapendekezo yaliyotolewa kabla. Na ndio maana mapendekezo hayo yaliweza kupitishwa kwa Maswi.....


Mbowe kuibuka na kubadilisha kabisa mwelekeo wa bunge, kama tutakuwa waungwana wengi wetu tutakiri kwamba ni kitu ambacho hatukukitegemea katika mazingira yale yaliyokuwa na majadiliano ya kiistaarabu !. Kwa kweli nashindwa kujua ushauri huu aliutoa wapi lakini kwa kweli maamuzi yake ya kusimama na kutishia kutoka yeye pamoja na wabunge wengine wa upinzani ndio ambayo yamesababisha CCM kulazimika kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kwa kweli kwa maoni yangu mimi imesababisha viongozi ambao tulitaka sana wawajibike (Muhongo, Werema na Maswi) wamependekezwa kuwajibishwa na Rais na vile vile imesababisha na viongozi wengine kuongezwa !


Katika maridhiano hayo kitu ambacho CCM wamepata kwa maoni yangu ni kubaki kwa Pinda tu.....lakini hivyo vichwa vingine vyote tumekula !. Mimi binafsi nimeridhika sana kwa matokeo haya 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wawajibishwe bwana tumechoka wananchi eeh mungu unawaona hawa tenda sawa tokana nawao walivyotenda hukumu nijuu yako hukumu hawa watu.

    ReplyDelete
  2. Hakuna kitu hapo zaidi ya watu kutia ndani mihela ya walala njaa tuu!

    ReplyDelete

Top Post Ad