Audio: Msikilize Jide Akithibitisha Rasmi kuwa Amemuacha Gadner

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe
kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G
Habash imevunjika.
Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha
Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye
uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya
kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa
akiteswa.
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa
siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi
kwenye vyombo vya habari.
“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu
ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye
media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote
ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha
yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote
wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu
anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee
kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na
privacy. Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza
kuelezea mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au
mume wake alimfanya hivi, sidhani kama kuna mtu yeyote
anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele za
watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja
wa watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili.
“Swali nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil
Haule, mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”
Isikilize interview hiyo hapo chini.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. apige kinya nini? cha ajabu ni kipi hapo? huwezi kuvumilia mateso et una mume, mume jina wa nini jamaniiiiiiiii? tuwe na msimamo kaona hawezi bas mwacheni aangalie mbele, kwanza wanaume wengi sasa ni matatizo tu hakuna jipya songa mbele Jide

    ReplyDelete
  2. Wanawake wengine huwa ni provacative kwa wanaume zao hilo ni lazima tulikubali. Inatokea hata mwanaume umfanyie nini huyo mwanamke lakini bado atakufanyia madharau na vitimbi chungu mzima.

    ReplyDelete

Top Post Ad