Baada ya Wema Sepetu Kumwaga Diamond, Mama Wema Afanya Sherehe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CHEREKO chereko! Siku chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu kama ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo, Ijumaa Wikienda linashuka nayo mstari kwa mstari.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.

“Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar,” kilisema chanzo hicho.

SHEREHE ILIVYOKUWA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ‘menu’ ya ukweli kabisa, wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria.

“Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake, wakafungua shampeni, wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini,” kilisema chanzo hicho.


MAMA NA CHUKI YA MUDA MREFU
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu motomoto kuwa, mama Wema alipiga cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa muda mrefu.

“Mama Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa na mwanaye.”


MAMA WEMA ANENA
Baada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga Diamond.
“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu,” alisema mama Wema.

TUJIKUMBUSHE
Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali walimwagana, wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo, wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema, sasa  wamemwagana tena.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UONGO UTAWASAIDIA NINI?

    ReplyDelete
  2. Mama Wema hawezi mpenda Dai anataka mwanawe awe na mapedeshee wanaokata mkwanja na yeye anufaike sasa Chibu mwenzangu yeye mwenyewe antengeneza maisha yake!

    ReplyDelete
  3. Huyu mama shangungu tu kwendraa chefuuu.kichwa chake kimejaa tope.na chibu hio sio familia yakuoa wala hao niwakutumiwa tu.hatahao mapedeshee wanamtumia tu.

    ReplyDelete
  4. Sio hivyo Jamani Twende mbele turudi nyumba diamond anampotezea muda wema kabisaaaa,maendeleo ya wema zero,sio Kama alivyokuwa Na Clement ,Penny ebu rudi uchukue Mzigo wako Wema kajichokea mtoto Wa watu.aruuuu bora wema umeamka.

    ReplyDelete
  5. kwanini ameshindwa nayeye amemchukuwa kwa penny kwa vishindo .uzuri siyo sura uzuri ni tabia maendeleo ya wema zero kwa sababu akili yake ni zero hajasoma tizama wenye akili wamefika wapi yeye akili yake na nyiye mashabiki wake ndiyo mnamdanganya kama yeye ni mzuri uzuri tabia sio sura yeye anataka kila siku diamond ampe pesa za kuleweya afanye kazi hata diamond anafanya kazi haokoti barabarani kazi siyo aibu aibu kuiba na kuuza ngono

    ReplyDelete
  6. Mdau moet baridiii inakufwata ulipo umeongea point sana.wanawake wenye kujielewa kichwani wanajulikana huyu madam wao wacha ajione mzuri nafsini kwake.ila kwabongo hii hizo pushapu anazohemewa na wanaume ndiomaana milima na mabonde inatokea mwilini mwake.namama sasa kampata anamtumiajee.clemee Rudi umalizie fupa lako ilaukiwa naakili hapo usigeuke nyuma huo niuwanja wa mazoezi wawatu.

    ReplyDelete

Top Post Ad