Waziri Nyalandu: Nitachukua Uamuzi Mgumu Muda Ukifika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema anaamini kuwa rais ajaye wa Tanzania, atakuwa ni kijana na kusema kwamba kila zama zina kitabu chake.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili hivi karibuni, waziri huyo alisema kuwa itakuwa ni kosa iwapo Rais Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa mtu mwenye umri unaofanana naye.

Nyalandu alibainisha kwamba wakati ukifika, atatangaza iwapo atagombea urais au kuendelea kugombea ubunge katika jimbo lake la Singida Kaskazini.

“Ukifika wakati ni lazima kubadilishana vijiti. Ni lazima kizazi kinachomaliza muda wake, kikabidhi kijiti kwa kizazi kinachofuata. Ni wazi mtu mwenye umri unaofanana na kiongozi anayeondoka madarakani hana nafasi,” alisema Nyalandu akiongeza:

“Kijiti hiki anachokiacha Jakaya Kikwete, aliachiwa na kaka yake Rais Benjamin Mkapa na Mkapa naye aliachiwa kijiti na kaka yake Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye ndiye alisema kila zama na kitabu chake.”

Alieleza kuwa huo ni uhalisia wa maisha na kwamba ni lazima kila mtu kukubali hivyo.

“Sasa tunahangaika kuandika hitimisho la zama za Rais Kikwete, ndiyo sisi tunapambana kuhakikisha tunakomesha ujangili na wengine wanafanya kazi nyingine. Haya yakikamilika ni zama zake (Rais Kikwete), zimekamilika,” alisema Nyalandu.

Alifafanua: “Rais Kikwete atakabidhi kitabu kwa zama nyingine na sharti akabidhi kijiti kwa kizazi kinachofuata. Haitawezekana ikiwa atakabidhi kijiti kwa kizazi chake hichohicho. Ni kosa kurudia zama zilizopita.”

Nyalandu alisema kuwa ni vyema mtu yeyote mwenye umri unaofanana na kiongozi anayeondoka madarakani akasahau kupewa kijiti kwani historia na hata maandiko ya Mungu vipo tofauti.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MICHOSHOO KUTWA KUWAZA UFISADI NA MUFILISI WA HILI TAIFA

    ReplyDelete
  2. hivi huuu uraisi ni kwamba unachaguliwa na watuuu? au unajiamulia mwenyewe? haya majamaaa vipi? nani kamwambia huyu jamaa afikirie anachokisema?

    ReplyDelete
  3. hao vijana wanaopiga wazee jamani itakua nchi au balaa kwakweli urais unatakiwa hekima na ujasiri wa hali ya juu kwani vijana wa hapa kwetu bado kufikia kuwa rais kwani wana jaziba siszo kuwa na maana na sitarehe nyingi

    ReplyDelete
  4. vijana hawa wapumbavu kabisa, hamna kitu hapo, c unaona wanapiga mpaka baba zao.

    ReplyDelete

Top Post Ad