Lemutuz: Kwanini Waziri Mama Tibaijuka ni lazima Ajiuzulu sasa Au Aondolewe na Mh. Rais!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

kwenye Press Conference yake amesema mengi sana lakini hakuna la maana wala msingi alilolisema la kumnusuru na hasa baada ya Mwanasheria Mkuu Werema ambaye hakutajwa kupokea senti tano za Escrow alipotangulia mwenyewe badala ya kumsubiri Rais kama anavyotaka kufanya Waziri Tibaijuka, ninasema hivi:-

1. Waziri alikuwa UN kwa muda mrefu sana anajua maadili ya UN kwamba ukituhumiwa tu kupokea hata senti tano nje ya kazi yako unafukuzuwa kazi siku hiyo hiyo, ndio maana Ban Ki Moon amesema haamini kwamba ni kweli kuwa Waziri Tibaijuka amepokea hizo pesa. Now understand hakusema haamini kwamba ameiba isipokuwa haamini kwamba amepokea hizo pesa, WHY? anajua kwamba huyu Mama baada ya muda wote aliokuwa UN anajua better kuhusu kupokea anything nje ya kazi.

2. Waziri Tibaijuka jana kuna kosa moja kubwa sana alilolifanya nalo ni kutooonyesha the media record ya tabia yake ya kupokea pesa za misaada, alitakiwa awaonyeshe waandishi wa habari historia yake ya kupokea misaada akiwa Waziri na kabla hajawa Waziri at least angekuwa na upenyo wa kutokea kwamba ni tabia yake toka akiwa UN kupokea misaada ya pesa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa sio hapa tu hata alipokuwa huko UN. Sasa kwa kushindwa kuonyesha hilo anakuwa anaelea elea na utetezi wake kwamba zilikujwa ni pesa za misaada ya Shule.

3. Pesa za Escrow alizozipokea kuna Makanisa na MaaAskofu waliozikataa, kwa mfano Kanisa la Saint Peters lilizikataa pesa hizo meaning kwamba Kanisa lilishituka kwamba process haiko sawa sasa ina maana Kanisa linaweza kuwa na smart judgement kuliko Professor Anna Tibaijuka WAziri wa Jamhuri na former UN Boss? Haingii akilini, uchunguzi ulkiofikishwa bungeni umeonyesha Waziri alipokea pesa hizo 1.6 Billion na kuziingiza kwenye account ya shule anayioisema na siku mbili later akazitoa bila Shule kujua wala kuidhinishwa na bodi ya Shule WHY? 

- Kwa kumalizia nasema hivi Waziri Tibaijuka aondoke sasa kabla ya Rais hajamuondoa maana hawezi kumuacha no way itakuwa ni Banana Republic Taifa ambalo Mawaziri wanaruhusiwa kupokea Billions kutoka kwa wafanya biashara bila kumuarifu anybody are you kidding me or what? Nashangaa mpaka sasa nafsi yake haimsuti kwamba MWanasheria Mkuu ambaye hakupokea senti tano amejiondoa mwenyewe kuwajibika na yeye aliyepokea anadai hana makosa please, enough Wananchi wamechishwa na hizi longo longo huyu mama kuna mnaoheshimiana naye mnasoma hapa mwambieni alichokifanya jana kwenye media ni sawa sawa na ile Press ya Miss Tanzania nothing personal lakini hata hiki Chama Cha Mapinduzi mnakimaliza wenyewe I mean Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya Nyerere usikike umepokea Billion kutoka mfanya biashara hivi kweli kungekuwa na kesi tena? Alikuwa anasema nini pale mtumzima mwenye elimu kubwa kuliko Wananchi wengi wa Taifa hili? Halafu na nyie media ya bongo kwa nini huwa hamuulizi maswali serious?

- Alipokuwa anawataja kina Rais Mkapa na Mzee Mengi kuwahi kumchangia mngemuuliza alipokuwa UN aliwahi kuchangiwa na je kabla hajwa Waziri Mkapa na Mengi waliwahi kumchangia?

- MAMA TIBAIJUKA JIUZULU TU UKINUSURU CCM CHAMA CHA MAPINDUZI HUWEZI KUWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NA WAZIRI WA JAMHURI UKAANZA KUPOKEA MISAADA YA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA NCHINI NI MAKOSA MAKUBWA SANA JIUZULU NOW, IFIKE MAHALI VIONGOZI WA TAIFA MCHAGUE KUWA VIONGOZI AU KUPOKEA MISAADA YA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA ILA HAMUWEZI KUCHANGANYA VYOTE, HAPANA SISI WANANCHI HATUTAWARUHUSU!!

Le Mutuz
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HONGERA SAAAANA LE MUTUZ!!! HAYO ULIYOYASEMA NI SAWA SAWA KABISA MIYE NILISHASEMA TOKA MWANZO MAMA ACHIA NGAZI UMECHAFUKAAA

    ReplyDelete
  2. Wezi watupu ata wewe lemetuz unapinga nn wakati ni mahypocrite mliokubuhu,si ndio nyie ccm wote?pambavu! !!!

    ReplyDelete
  3. kwa nini aachie wakati wizi rushwa na ufisadi ni mfumo wa nchi na wananchi wameukubali?

    ReplyDelete
  4. Kwani Mama hizo ulizo chukua hazikutoshi? Mama jiheshimu afu chukua hatua aibu hiyo.

    ReplyDelete
  5. Le mutuz ni mpotoshaji mkubwa sana juu ya hela ya escrow,Huyu mama hajaiba hela ya escrow yeye kapewa hela ambayo source yake ni escrow,wezi ni wale waliyoitoa hiyo hela, hii aina tofauti na mtu kutoa sadaka kanisani au msikitini je wachungaji wanaulizi source ya sadaka(hela) waumini anapozitoa, source yaweza kuwa ni mauzo ya drugs etc. Hata report ya CAG haija onesha sehemu yoyote ile yeye ameusika na uchotaji wa pesa

    ReplyDelete
  6. Leo Le Mutuz umeongea point! sasa inatakiwa siku zotu utuimpress wasomaji wako kwa kucoment issues serious seriously! ni kweli huyu mama atoke hafai!

    ReplyDelete
  7. Huyu mama analeta jeuri za Kihaya, hivi bongo hii mtu akudipositie 1.6 b eti ni msaada wa shule? no way! kama huyo mtu ni generous kiasi hicho kwanini asisaidie shule za walalahoi za kata? au basi vituo vya watoto yatima? au angesema ni co investor ametoa capital yake tungeelewa! Watanzania sasa tumeamka hatudanganyiki kirahisi mama Tibaijuka! Umetoka zako UN watu wakaona unafaa kulisaidia taifa kumbe siyo! Hata ile press conference eti Mimi sijiuzuru! aibu gani hii we mama! tena kwa jeuri zote kabisa! Puuh!

    ReplyDelete

Top Post Ad