Muhongo - Watanzania Wawekezaji Juice Ndio Wanaoongoza kwa Utajiri Kuliko Wachimba Madini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa nishati na madini Profesa Muhongo moja ya tamko ambalo linaonekana kumshusha hadhi kama msomi asiyefikiria kwanza nini anakitamka na kufanyia utafiti ni pale aliposema watanzania uwezo wao ni kuwekeza kwenye juice badala ya nishati na madini. Kwa mtazamo wake utajiri upo zaidi katika uwekezaji wa madini badala ya manufacturing.

Hawa aliowakandia uwekezaji katika juice ndio matajiri wakubwa latika list ya matajiri 50 Afrika ambao wengi wao wanajihusisha katika biashara ya vinywaji baridi isipokuwa Rostam Aziz ambaye ana hisa kubwa kwenye kampuni ya Vodacom.

Katika mataifa mbalimbali duniani matajiri wakubwa ni wamiliki wa viwanda, retail and whole sales, real estate na teknolojia ya habari na mawasiliano, bado sijashuhudia matajiri wakubwa wanaotegemea biashara ya bahati nasibu ya madini. Wengi wanaosifika kuwa matajiri wa kutokana na madini ni utajiri wa kufikirika usioonekana wala kufanyiwa tathmini kibiashara kupima mapato yao na vitendea kazi vyao kitakwimu.

Muhongo amedhalilisha taaluma yake, na kauli yake haionyeshi upeo wa msomi zaidi ya kutumia ukali na majigambo bila hoja zenye kuleta ukweli kwa anachoongelea. Anaonekana kutumia nafasi ya hadhi yake kama kinga kama alivyokuwa Werema ambaye akiishiwa hoja bungeni alitaka kuwa tayari kupambana kwa masumbwi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unafikiri Elimu ya kukaa darasani ndio kuwa na akili nyingi, kwanza inadumaza, upeo, ekima busara, hana bisara hata kidogo, hivi hawaioni nchi yao ilivyonamatatizo lukuki, wao wanaona raha tu, ka kuwa hela za walipa kodi zimerundikana pale basi wanajichotea wanavyotaka. jamaani ujinga na umbumbu, sio mpaka uwe na elimu ya darasani ndio ukazani wewe si mbumbu, hata huyu ni mbumbu pia wa mawazo, busara, kiakili yaani kujielewa wewe mwenyewe na Taifa lako, waliokukabidhi madaraka ya kazi yako, na haya only in Africa, ndio maana bara alipigi hatua hili, kutokana na watu kama hawa, mbumbu wa mawazo, ya kuchanganua, shame on you unaejita una elimu ya kutosha. ili muwakandamize wenzenu, stupid slave mind

    ReplyDelete
  2. Sio mwakilishi wa wasomi wa kweli. Ni ujinga wake tu na kalewa hel. Muulizeni nani anampa hicho kiburi.

    ReplyDelete
  3. majigambo huwa hayaji hivi hivi blogger. Ukiongelea kitaaluma Prof. Muhongo katusaidia sana watanzania kuelewa uwekezaji wa mafuta na gesi jinsi ulivyo. Kwa kuwa hakupita mtaa kwa mtaa kukuelewesha basi hata ulichopost kitazidi kuwa mada hata mwakani ila ni kutaka kuibua hisia tu za watu. Ingependeza kama ungeonesha mianya ya mtanzania kuwekeza ambayo Prof katuzibia. Fursa zipo kwa watanzania katika swala la kuwahudumia wanaochimba visima baharini au porini (kama chakula,maji/juice,sabuni,store/warehouse,stationary.....n.k)

    ReplyDelete
  4. nimeamini nabii hakubaliki kwao. Prof Muhongo ataeleweka miaka 20 mbele kama tunavyorudia kuangalia na kusikiliza rekodi za Baba wa Taifa. Mimi bado sijaona mtu ambae kafanya kwa vitendo vitu ambavyo Prof kasema watanzania hatuviwezi. Ni rahisi kufikiri unamdhalilisha mtu bila kujua unajidhalilisha. Watanzania tubadilike hatuwezi kuendelea kusubiri mambo yasemwe ndio tuanze kuongea hayo sio maendeleo. tutaendelea kusubiri. Hasa vijana. Asante Prof kwa ujasiri wako maana kwa mawazo ya wengi wasioelewa hayana maisha marefu kuweza kuyabaini. Mzalendo wa kweli.

    ReplyDelete
  5. Naunga mkono Hoja mengi hana hadhi ya kuchimba madini ya gas hiyo media tu kuihudumia ni mshike mshike watu wanafanya kazi kama vibarua more than 3 years then ataweza biashara ya gas ambayo ina risk kubwa kiuendeshaji kama milipuko n.k hivyo inahitaji white colors employee ambao watamudu kuendesha pamoja na vifaa vya kisasa sasa ujanja ujanja wa huyo tapeli wa kimangi hapo hawezi chomoka aache tamaa afocus kwenye vitu vyake tu kama nipashe na dawa za meno hito tanzania one yenyewe hatujaona output ya maana kwa watanzania heri hata Barick au GGM. ni hayo tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wote mmeongea usenge tu. Hakuna hata mmoja anayejua alichokisema. Ni bora mambo ya Ngoswe aachiwe Ngoswe mwenyewe.

      Delete
    2. yamekuchanganya mambo ya kitaalam...... ukweli unauma toka enzi, kinga yako iliyobaki ni matusi.

      Delete
  6. Hao matakjiri wa Africa mbona hawawezi kujiunga wote watengeneze kampuni moja naowakachimbe hiyo gesi kama wana hera? Bali tajili mmoja ndo anataka wakati pesa yake haitoshi hata kunnua mashine moja ya kuchimba, bado ghalama za utafiti. Namshangaa sana yule mzee kama anayo pesa aende wizarani MUHONGO alitoa ghalama za utafiti navitaru na akasema mwenye kuweza aende yeye bado anasubuili nini, kazi kuendeleza umbea, kama amedhalilishwa kweli ajitokeze ili tujue kama kweli anazo hizo pesa, sio kusubili vilivyo mezani tayari kuliwa

    ReplyDelete

Top Post Ad