Simba Napo Kimenuka, Yamtimua Kocha Patrick Phiri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Yanga sasa ni Simba, Phiri na bechi lake lote wametimuliwa Simba na kesho atapewa barua na haki zake za msingi zitafuatia.
MSERBIA GORAN ambaye alishawahi kuifundisha POLICE ya RWANDA ndiye rasmi kocha wa Simba na atasain mkataba siku ya j5 jioni.
Mserbia huyo atasaidiwa na kocha kutoka Rwanda anaitwa JEAN MARIE NTAGAWABILA.
Hiyo ndiyo habari ya mtaa leo

Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa.

Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.

"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.

"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.

Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.

"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania ni nchi ya kwanza duniani kwa kufukuza makocha.

    ReplyDelete
  2. msindikizeni airport sasa nyie mnajua kumpokea tu!!!! sukari taaaaaaammmmm!!! pigaaaa hayooooo!

    ReplyDelete

Top Post Ad