Baada ya Kumfukuza Kocha Hali ya hewa Simba Sports Club Bado si Nzuri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Huku wakiwa na kumbukumbu ya kufugwa mchezo wao wa mwisho wa ligi kuuu ya Tanzania bara, wekundu wa msimbazi Simba Sports Club hii leo waliendelea na mkosi wao baada ya kukubali kipigo cha 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa kombe la Mapinduzi uliopigwa usiku huu.
Simba wakiwa na kikosi cha vijana ambacho kilikuwa chini ya Kocha Suleiman Matola huku wakiwa wanatazamwa na kocha wao mpya Goran Kopunovic aliyekuwa jukwaani akifuatilia mchezo huo, walishindwa kuelewana na kuwaruhusu Mtibwa kufunga bao kwenye dakika ya 41 ya mchezo mfungaji akiwa kiungo wao wa zamani, Henry Joseph.

Bao hilo lilifungwa baada ya kona ambayo iliunganishwa kwa kichwa na Ali Shomari kabla ya Henry Joseph kumalizia kwa shuti hafifu ambalo lilishindwa kuzuiwa na mabeki wa Simba na kipa wao Manyika Junior.

Mabadiliko yaliyofanyika kwenye kipindi cha pili ya kuwaingiza Danny Serunkumma na Jonas Mkude pamoja na Shaban Kisiga hayakutosha kuirudisha Simba mchezoni na hadi kipindi cha pili kinamalizika kuashiria mwisho wa mchezo huo Simba ilifungwa 1-0.
Michuano ya kombe la Mapinduzi inafanyika visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Mapinduzi ya visiwa vya Zanzibar na michezo yote imekuwa ikionyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam Tv.
~Millard Ayo

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad