Diamond Atupiwa Jini, LAMPATA mama Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diamond Akiwa na Mama yake Mzazi
Imevuja! Kuna madai kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametupiwa jini lakini likamkosa na kumpata mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ kisha kumsababishia ‘gonjwa’ la ajabu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, watu wanaodaiwa kuwa ni wabaya wa Diamond (Anti-Diamond) walimtupia jini staa huyo lakini bahati nzuri likamkosa na kwa bahati mbaya likampata mama yake ambaye alipata ugonjwa wa kupooza ghafla.

“Ujue kumekuwa na sintofahamu kwa muda mrefu juu ya ugonjwa wa mama Diamond lakini habari za uhakika ni kwamba, mama Diamond yupo hoi baada ya kutupiwa jini ambalo mlengwa wake alikuwa Diamond.

“Mungu tu hakupenda limpate Diamond lakini inasemekana kwamba jini hilo ni hatari endapo lingempata Diamond kwa jinsi lilivyokuwa, basi pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND ALIJUA ‘MCHEZO’ HUO?
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, Diamond alijua kwamba mama yake ametupiwa jini ndiyo maana alikuwa akisuasua kutoa uamuzi wa kumuwahisha nchini India kwa matibabu ya hospitali.
“Diamond alijua kuhusu mpango huo wa wabaya wake kutaka kummaliza kishirikina ndiyo maana hakutaka kumkimbiza haraka hospitali na badala yake alijikita kwenye swala na dua kwani yeye anaamini katika dini zaidi,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, baada ya kutafakari kwa umakini wa hali ya juu, imeelezwa kwamba, Diamond alilazimika kumpeleka mama yake nchini India na kupatiwa matibabu kisha kurejea nchini.

ALIRUDI MZIMA
Kwa mujibu wa ndugu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, hivi karibuni (kabla ya Valentine’s Day), mama Diamond alirejea nchini akiwa na afya njema lakini siku chache baadaye alizidiwa tena na kurudishwa India huku ndugu wakijawa na hofu.

“Alirudi Bongo lakini hakukaa sana akazidiwa tena tukalazimika kumrudisha India kwani hali ilizidi kuwa mbaya. Tumekuwa hatutaki kueleza sana juu ya suala hili maana Diamond mwenyewe hapendi haya mambo yajulikane,” alisema ndugu huyo.

DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya chanzo hicho kuvujisha ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimvutia waya Diamond ambapo alikiri kwamba mama yake yupo India lakini hakutaka kulizungumzia zaidi eneo hilo badala yake akaanza kushusha lawama kwa wale aliodai wanamsema vibaya.

“Mama bado yuko kwenye matibabu nchini India na hali yake kusema kweli si nzuri, naomba hapo nisizungumzie sana. Kuhusu masuala ya kutupiwa jini, mimi namuamini Mungu, naamini mama atapona.
“Inaniuma kila siku ninaposikia watu wanaongea vitu ambavyo si kweli na kwa namna nyingine nashindwa kujibu vitu ambavyo mwenyewe sivijui hivyo yote namwachia Mungu, maana yeye ndiye jibu la yote.

“Halafu pia kuna muda ufike, watu wawe wanafahamu mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, wasiwe wananijazia vitu utafikiri mimi sina moyo, wawe waelewa, sipo katika kipindi kizuri kwa sasa na si kila kitu wanachosikia au kuona lazima mimi nikizungumzie, kuna mambo mengine ni ya ndani ya ukoo na yako juu yangu sana, hivyo ukiona kimya simaanishi kuna watu nimewadharau,” alisema Diamond.

TUMEFIKAJE HAPO?
Hivi karibuni kuliibuka madai kwamba kwa makusudi Diamond alishindwa kuhudhuria msiba wa baba Abdul Sykes ‘Dully’ na badala yake picha zikavuja zikimuonesha akiwa kisiwani Zanzibar na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari’ kitu ambacho mwenyewe alikikanusha.

“Si kila picha unayoiona katika mtandao wa kijamii basi itakuwa imepigwa muda huo, inaweza kuwekwa leo kumbe ni ya muda mrefu,” alisema Diamond.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha majini... hata irfiid watamshukia mama huyo... mwanamke gani wa kiisilamu tena mzazi asiojistiri? bila sitara na taqwa ya mja kwa mungu wake.... wacha majini hata iblis hutengeneza makazi maana hana tafauti na jalala...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmh,una hasira.

      Delete
    2. yaani ni maneno yanaonesha wivu wa kupindukia!!!

      Delete
    3. Hizo hasira!!!!! hmmm tena aswa. Aliyepewa kapewa nawe ngoja ridhiki yako kama yaja, ikiwa kwa mtoto wako haya, lakini iwe halali, sio ya wizi au kifisadi, ikiwa nae mwanao atajaliwa saut,i ni kipaji chake sasa jasho kumtoka, kwa kuitumia hiyo sauti

      Delete
  2. pole mama utapona,nazidi kukuombea kwa mungu

    ReplyDelete
  3. Are you for really you must really lost your mind and a big hater.how could you say that did you just woke up.are you a really human being talking about someone mother like that do you have a mother seriously l can't belive what l'm reading up there.wow tanzania nakupenda but we are going in a wrong direction mpa watu wanakuwa na chuki hivi hater mkubwa we may you are among of those waliyomtupia hayo majini???

    ReplyDelete
  4. Mh shetani ndo alivyo kanumba alimpenda mama yake lkn diomond anajipenda mwenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous 3:05 unamaanisha nin?

      Delete
    2. Hizo photo mnazo shinda mkipost kumbuken ni photo zenye zaonyesha unajienjoy so hata kama siza wakati huo na umeweka wakati unaosemekana uko huko nan ataamin unapitia shida na nstarehe tunaona. Stop childish Zari ni mama na anaakili yakuweza kufanya hata watu wengi wasijue kunaendeleea nin katika lif yenu ya kila siku

      Delete
  5. wewe anony wa kwanza acha kumjaji mama wa watu,kwani umeambiawa kujisitiri peke yake ndo unaenda peponi?na nyie mnaojisitiri ndio mafilauni wakubwa nyie nani asiwajue mbona mmejaa kitaani kwetu kazi kujisitiri na kuzama gesti na baibui zenu hizo.

    ReplyDelete
  6. Weye nani waku jugde bina adamuwenziyo weye una ujuwa mwisho wako .pili kama weye kweli ni muislam hupashwi kusema hivo kwanza ungekimstiri mama wa mwenziyo kisha ukamuombeya shifaa siyo kumkashif bina adamu.
    Ivo tanzania nzima anakaye fanya makosa ni diamond tuu aliye penda ni diamond tuu wacheni wivu uta wauwa

    ReplyDelete
  7. Diamond badilika japo kidogo mdogo wangu wote tunatenda makosa hakuna binadamu aliye mkamilifu ila kutenda dhambi za dhahiri siyo vizuri!

    ReplyDelete
  8. CHUKI NA HASIRA YA MAISHA YA KISWAHILI BILA MAFANIKIO NDIO HAYO MAWAZOALIOKUWA NAYO HUYO MTUKANA MATUSI MACHAFU KWA MAMA WA DIAMOND!--- KAMA MTU KATOKA NI MIPANGO YA MUNGU KWANI HAPO TANZANIA KUNA WANGAPI VIJANA WANAENJOY ZAIDI YA HUYO KIJANA NASSEB, MBONA HAMUWAOMBIE MABAYA MAFISADI WANAOTEKETEZA PESA ZA UMMA PAMOJA NA WEWE MTUKANA MAMA ZA WATU, MNAWASIFIA TU NGELEJA ANA PESA ,MBONA HAJATUKANIWA MAMA YAKE?

    ACHENI WIVU WA KIJINGA KAMA DIOMOND KAKUSHINDA WEWE KUBALI MATOKEO TU SIO KUMLANI KIASI HICHO WEWE SIO MUNGU NA WEWE NDIO UTAANZA KUFA MAPEMA KABLA YAKE HUYO KIJANA UNAMUONA KANA KWAMBA MAMA YAKE HAFAI, SWAIN MKUBWA WEE MSHENZI NINYI NDIO MNAOKAA KUTENGENEZA MAJINI YA KUWAZURU WATU ILI KUFUBISHA MAENDELEO,.

    KWANINI MSIMUUNGE MKONO AZIDI KUENDELEA ZAIDI NA ZAIDI, ATUPEPERUSHIE BENDERA YA NCHI ,KAMA TUNAVYOANZA KUJULIKANA KIMUZIKI DUNIANI ,WEWE UNAMUOMBEA MABAYA. HABITHI MCHAWI MKUBWA .

    KAMA NA WEWE NI MIONGONI MWA MLIOTENGENEZA HILO JINI BASI WAKO WENGINE WENYE UWEZO WA KULITOA NA KULIUA.

    WATANZANIA TUCHE ROHO MBAYA-

    ReplyDelete

Top Post Ad