Msanii Temba Kutoka TMK Wanaume Apandishwa Mahakamani kwa Kutishia Kuua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Nipashe, Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.
Mheshimiwa Temba alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa amefungwa pingu chi ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe.

Aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya kusomewa mashitaka yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya Makosa ya Jinai.

Akisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa Januari 28, mwaka huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion Iiliyopo Temeke jijini Dae es salaam, mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu Godrey Deogratius ama Sulla.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo nje kwa dhamana.

Hakimu Frank alisema kesi hiyo itasikiliza ushahidi March 11, mwaka huu,. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mshitakiwa alifikishwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe akituhumiwa kutishia kumchoma kisu mlalamikaji kwa madai ya kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mke wa msanii huyo.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu mlalamikaji huku akijua ni kinyume na sheria.

Source:Nipashe
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad