Uteuzi wa Makonda ni fimbo kwa mafisadi. Asibezwe, anaweza na apewe nguvu na moyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Uteuzi wa Makonda ni fimbo kwa mafisadi.Asibezwe anaweza.

Anaitwa Paul Makonda.Ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Uvccm.Kijana mdogo mwenye ujasiri wa kipekee asiyeogopa kejeli,dharau na fitna za mafisadi.Kwasasa ndio Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Jamii ya wenye akili inashangaa wanaobeza uteuzi wa rais kwa Paul Makonda.Inawashangaa wanaomponda Paul Makonda.Haijajulikana hadi sasa nia na sababu zenye mashiko zinazotumika kumchafua Paul Makonda.Vijana wanaombeza ndio haohao wanaoomba kila siku kuwa vijana wapewe nafasi katika vyombo vya maamuzi.

Kumponda Paul Makonda ni kudharau uteuzi wa rais wa nchi.Rais anatambua umuhimu wa vijana kupewa nafasi.Anatoa fursa kwa vijana.Hili ni jambo la kupongezwa sana.Ni hatua kubwa na nzuri kwa ukuwaji wa demokrasia nchini.

Paul Makonda kaaminiwa.Mnalalamika kila siku kuwa kina January na Kigwangallah au Mwigulu wasibezwe tena wao wanaomba nafasi kubwa ya urais.Lakini Paul Makonda kupewa Udc mnaona kama kapendelewa na hawezi.Sisi tunaamini Paul Makonda anaweza na wilaya aliyopewa aiongoze ataimudu,aungwe mkono kwa asilimia mia moja.

Kelele za mafisadi zisiondoe imani kwa vijana wasiowaunga mkono.Paul Makonda anapinga ufisadi.Ni jasiri.Mpiganaji wa kweli dhidi ya maovu.Kambi za urais zisiwapotoshe.Wanaomsema hovyo wamepoteza dira ya kisiasa na kimaisha.Wana political stress isiyotibika inayotokana na kukosa maadili ya uongozi na kisiasa.

Abarikiwe Paul Makonda.Abarikiwe aliyemteua.Ibarikiwe Ccm.Ibarikiwe Tanzania.Ibarikiwe Kinondoni.Viva Paul Makonda "Jembe".
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ina maana Mafisadi wote wa Tanzania wako Kinondoni kwa hiyo atawazuia kulitia nafasi ya Ukuu wa Wilaya ikumbukwe suala la Rushwa linahitaji nguvu ya pamoja wala si kiongozi mmoja kama ni suala la mtu mmoja mbona uuaji wa walemavu wa ngozi maarufu Albino tunalaumiwa na Umoja wa Mataifa naamini kila mkuu wa Wilaya aliyeteuliwa ziko ahadi za kukamilishwa Ilani ya Uchaguzi uliopita kuna ukamilishaji wa maabara tatu shule za sekondari kabla ya Uchaguzi mkuu sasa suala la kupambana na wagombea Urais sionimantiki yake hapa

    ReplyDelete
  2. we ngoja tu aanze kutafuta visa kabisa pa kwenda kuishi

    ReplyDelete

Top Post Ad