Ivo Mapunda : Mkiniiga Staili ya Kitaulo..Naingia na Blanketi Kabisa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KIPA wa Simba, Ivo Mapunda huwa haishiwi vituko jamani, eti kwa sababu idadi ya makipa wanaobeba mataulo Ligi Kuu Bara imekuwa ikiongezeka, amesema kama watakuwa wengi, atabadilisha staili hiyo na sasa ataingia na blanketi uwanjani.

Ivo amekuwa kivutio kwenye mechi kutokana na staili yake hiyo ya kuingia na taulo uwanjani. Ni staili ambayo ilimpa umaarufu tangu alipokuwa anaichezea Gor Mahia ya Kenya japo imekuwa ikihusishwa na imani za kishirikina.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ivo alisema: “Hii staili ya taulo naipenda, lakini kwa sasa naona wanaobeba wamekuwa wengi, kama wataendelea kuzidi nitaibadilisha.

“Na kama nitabadili, badala ya taulo, sasa nitakuwa naingia uwanjani na blanketi, nikiwa na mwonekano mwingine.”

Kutokana na taulo hilo, amekuwa akiingia kwenye migogoro na wachezaji wa timu pinzani pamoja na waamuzi.

Ugomvi wao ni pale anapokuwa anataka kulitundika kwenye nyavu za goli, jambo ambalo wenyewe wanaona siyo sahihi na kumtaka aliweke chini na wanafikiri kuwa upo uchawi ingawa mwenyewe huwa anapinga suala hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAKUNA UCHAWI NI MBWEMBWE ZAKE TU

    ReplyDelete
  2. Masifa tu,, nae kaiga staili hiyo toka kwa makipa wengi tu Ulaya wanaobeba taulo!!!

    ReplyDelete
  3. Mbona dizaini ya vitaulo ipo toka wewe haujazaliwa watu hitumia hasa katika nchi zenye joto kali shauri ya kujifuta jasho kwa hiyo hapo hakuna mpya kabisaaaa japo mimi ni mpenzi mkubwa wa Simba Sports Club tangu enzi za akina Mambosasa Omary Chogo Kajole Haidary Abed upo hapo?

    ReplyDelete
  4. wala sio uchawi ni stye yake

    ReplyDelete

Top Post Ad