Nuh Mziwanda Anusurika Kupigwa Chupa na Shilole ambaye ni Mpenzi Wake.....Hili ni tukio la Pili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.

 

Katika tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda,ghafla sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa chupa ambayo ilikuwa ikimlenga msanii huyo bahati nzuri aliikwepa ikampiga jamaa mmoja lakini haikumjeruhi.

 

Baada ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie juu Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua kukaa pembeni peke yake na kuanza kulia.

 

 ‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli alileta fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu walikuwa kwenye sherehe hiyo.

 

Baada ya hapo msanii Quick Racka alimfuata Shilole na kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia chupa ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye aliikwepa ikapasuka chini.

 

Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu Shilole kumsomea mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo alikuwa amelala.

 

Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh Mziwanda kwa kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi karibuni alimpiga vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za viwanja vya Leaders na baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia vyombo vya habari na kuahidi kutompiga tena.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MMM SASA ANAKWENDA KUBAYA BAADA YA CHUPA KITAFUATA KISU!! NUH TAKE CARE!!!

    ReplyDelete
  2. wambea haoooooo wambea tuwape bambino mvae udaku,mngeongea mengine yapi kama huyo jamaa wa pembeni ya nuh haikumudhuru ko mziwanda ndo yangekua mengine heheheheheheheheheheheheheheheeeeeeee mtasutwa na vidogoloooooo Udaku Mashauzi

    ReplyDelete
  3. huyo kijana aache ujinga. aje nimpe kazi ya ukonda kwenye basi.

    ReplyDelete
  4. ujue nuhu naye anapashwa ajitambue bana kila mara anazalilishwa mpk lini hata kama ni kupenda ipo sk atakuua

    ReplyDelete
  5. Ni usenge tu,dogo atakuwa anapigwa sana ndani,achana na mama Malaya huyo,umeolewa wewe Nuh,mapenzi mapenzi kumbe ufala tu,bwege wewe.

    ReplyDelete
  6. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu je mademu wangapi wanadhalilishwa na wanaume kila siku toka enzi na enzi mpaka leo hii?Hilo hata hamuoni wala kulizungumzia

    ReplyDelete
  7. Wanyamwezi hutuko hivyo huyu cjui ni mnyamwezi mchanganyiko!!!!!!!!!!!!!!!nina wasi wasi

    ReplyDelete
  8. mh haya ya ngoswe mwachie ngoswe

    ReplyDelete
  9. Huyu baradhuli sijui anapewa Tigo ndio maaana kang'angania!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad