Sangoma Akamatwa na Kichwa Cha Mtu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati kamatakamata ya waganga wa kienyeji ikiendelea kupamba moto katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, mmoja amenaswa akiwa na viungo vya binadamu, kikiwemo kichwa ambacho bado kilikuwa na nywele zake.

 

Mganga huyo, Nyamizi Makunga (70), mkazi wa Kijiji cha Igurubi wilayani Igunga, Tabora, alitiwa mbaroni juzi. Mbali na viungo hivyo, pia alikutwa na vifaa vingine, zikiwemo nyara za serikali.

 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Igurubi, George Henry, alisema Makunga alikamatwa nyumbani kwake kutokana na msako mkali unaendelea kwa lengo la kuwabaini waganga wanaofanya ramli chonganishi.

 

Msako huo umetokana na kukithiri kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ambapo serikali katika kubaini chanzo, imekuwa ikisaka waganga wanaotuhumiwa kufanya ramli hizo.

 

Henry alisema polisi walifanikiwa kumnasa Makunga kutokana na taarifa kutoka kwa raia wema, ambapo walipofanya msako walikuta fuvu la kichwa la binadamu likiwa na nywele zake.

 

Mbali na fuvu hilo, polisi pia walikuta kipande cha mfupa wa binadamu, mkia wa nyumbu, gamba la kobe na ngozi za wanyama mbalimbali.

 

Wananchi wa Kijiji cha Igurubi, wamepongeza msako unaofanywa na polisi kuwatia mbaroni waganga ambao ndio chanzo cha kushamiri kwa mauaji ya albino.

 

Pia walisema kwa muda mrefu Makunga amekuwa kikwazo cha maendeleo kwenye eneo hilo kutokana na kufanya mambo kinyume na kwamba wananchi wamekuwa wakimwogopa.

 

Alipohojiwa, Makunga alikiri viungo hivyo ni vya binadamu na kuwa aliachiwa na baba yake ili kuendesha shughuli za uganga.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda, alithibitisha kukamatwa kwa mganga huyo akiwa na viungo vya binadamu.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WACHUKULIWE HATUA KALI SANA!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. YALE YALE, KUNA MZUNGU ALIKAMATWA NA KIOUNGO CHA MWANADAM, MZUNGU ALIKUWA MWENYEJI WA UBELIGIJI, AKAKAMATWA EARPOT, WATU WAKANDIKA MENGI, KWAMBA SIO KAWAIDA KWA HAPA KWETU, HAWA WAZUNGU WANA MAMBO YA AJABU SANA, HAYA SASA HMNA CHA MZUNGU WALA MWAFICA. KAMA BINADAMU UNA MAMBO YA AJABU NI AJABU TU, NA HUYU NAE NDIO HIVYO NI MWEUSI TENA SISI NDIO TUNAONGOZA KWA MABO YA AJABU

    ReplyDelete

Top Post Ad