Wakamatwa na Viungo vya Albino Mwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewakamata waganga wa kienyeji 55 wakiwa na viungo vya binadamu vikiwamo meno na nywele vinavyodaiwa kuwa ni vya watu wenye albino. Vitu vingine walivyokutwa navyo ni ngozi ya simba, nyumbu, mamba, vibuyu, njuga, vioo, shanga na debe tatu za bangi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema waganga hao walikamatwa katika wilaya za Mkoa wa Mwanza kwenye msako ulioanza juzi. Alisema katika msako huo wamefanikiwa kuwakamata waganga hao wanaodaiwa kupiga ramli chonganishi zinazosababisha kuchochea matukio ya mauaji kwa albino na vikongwe.

“Katika msako wa Jeshi la Polisi ulioanza juzi tumefanikiwa kuwatia mbaroni waganga wa jadi 55 ambapo kati yao tumewakuta na nywele, meno za watu wenye albino waliouawa katika matukio tofauti mkoani hapa,” Mlowala.

Kamanda huyo wa Polisi alisema waganga hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwamo kumiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria pamoja na viungo vya binadamu.

Mbali na tukio hilo, taarifa kutoka wilayani Misungwi zinaeleza kuwa watu wanne wamefikishwa kortini mjini hapa kwa tuhuma za kuuza mafuta maalumu ya ngozi yanayotumiwa na watu wenye albino. Mafuta hayo yenye thamani ya Sh milioni tano, ambayo yalitolewa na Hospitali ya Bugando kwa watoto wenye albino wilayani humo.

Chanzo. Gazeti la Mtanzania
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa waganga wanalitia aibu taifa letu dunianzima inatuona niwatu waajabi sana,hebu tuache amani zakishirikina sio kila mwenyepesa aliua mtu,tufanyeni kazi kwa bidii.Natukumbuke hatutaishi milele ktk hii dunia...

    ReplyDelete
  2. Weka segerea waganga wote kwa miaka 30 kudadadeki

    ReplyDelete
  3. Kwani waganga wanashida shida inatoka kwa watu wanaotafuta uongozi na utajiri wa lazima wakienda huko wanadanganywa kwamba walete viungo vya binadamu watu waache tamaa ya mali nauongozi wa kulazimisha na wa ganga watakosa kazi ya kufanya waganga wanataka pesa ya kula watu na usomi wao na vitambi wanadanganyika wanakalia vigoda nakudhamiria kuwaumiza watu wengine elimu walizo soma hazija wasaidia wanapotosha taifa kwa kitu kidogo laikin mwisho wenu upo muwe wa ganga au wewe unaeambiwa utafute kiungo cha binadamu mwenzio utakufa kifo kibaya sana bora utubu acha hiyo dhambi itakupeleka jehanamu....

    ReplyDelete

Top Post Ad