Wanaume Watatu Wanyongwa Mkoani Kilimanjaro na Kisha Maiti Zao Kutelekezwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu watatu wanaume wasiofahamika, wamekutwa wamekufa na kutelekezwa maeneo ya Mjohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, huku miili yao ikionesha majeraha maeneo tofauti pamoja na kuvuja damu nyingi puani.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela (pichani) alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema ametuma maofisa wake eneo la tukio na taarifa rasmi ataitoa itakapokamilika.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu hao wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 28 na 32 wanadhaniwa ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mirerani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa maeneo ilipokutwa miili hiyo ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao miili hiyo ilikutwa eneo jirani na alipouawa bilionea wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya aliyeuawa kupigwa risasi kifuani.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema askari kutoka kituo cha Bomang'ombe walifika eneo la tukio majira ya saa 3:00 za asubuhi na kufanya uchunguzi katika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya vijana hao
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad