Alikiba ni Mmoja ya Mwanamuziki Mzuri Ambaye ana Management iliyoshindwa Kulikabili Soko la Muziki?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni ukweli ulio wazi kabisa Alikiba ni mmoja wa waimbaji/wanamuziki bora kabisa na mwenye kipaji cha aina yake hasa kuimba!

Ni wazi soko la muziki limebadilika sana na limekuwa na ushindani wa hali ya juu na pengine uwezo wa msanii unaweza usipimwe kwa kipaji chake bali uwezo wake wa kulikabili soko na kuendana na mahitaji ya soko la muziki! Na hapa kwenye mipango ndipo watu hushikana uchawi na kuanza kutuhumia ooh fulani ana bebwa ooh fulani anatumia nguvu za giza ..kumbe muda mwingine ni mipango tuu...
kuna jamaa wa futuhi husema "Mjini mipango.

Nami naamini soko hili hasa la sasa lina hitaji mipango na uthubutu wa hali ya juu kinyume na hapo soko litakushinda!

Alikiba ni mmoja ya wasanii wenye uwezo mkubwa sana na mwenye ushawishi sokoni lakini naamini ni mmoja wa wasanii mwenye management mbovu na iliyo choka kufikiri kabisa!
Management ya Alikiba haijawai kumbadilisha alikiba wala kumfanya Alikiba kuwa msanii mkubwa kama matarajio ya watu!

Wakati Alikiba anarudi nilitegemea atarudi huku akiwa amejiandaa kulikabili soko la muziki ambalo kwa sasa lina changamoto nyingi na halitegemei kipaji tuu!

Hivi management ya Alikiba haifahamu kuwa kwa sasa Video ina mtangaza msanii kuliko audio?
Hivi management ya Alikiba imeshindwa kumpandisha thamani Alikiba?
Hivi kweli Alikiba nae hadi sasa ana stahili kujumuishwa kwenye show zisizo na tija hasa zile zinazo onekana kabisa hazilipi?
Tangu Alikiba amerudi sijaona cha kipekee ambacho amerudi nacho kuweza kupambana na soko la muziki na ukweli ni kwamba Alikiba hakujipanga au kuna tatizo kubwa kwenye management yake!

Kusema kweli ni wazi ana hitaji kuitazama upya management yake pengine kuibadilisha kabisa maana haina tija kwakwe na ina mdanganya sana!
Hivi Alikiba na management yake wameshindwa kujua kuwa video inafanya wimbo huduma milele?

Pengine sio dhambi na sijawai kuhisi ni dhambi kuiga kwa wengine...kuanzia thamani ya show na kumbrand msanii na bila shaka mashabiki wa Alikiba wanatamani kuona Alikiba anaonekana kuwa ni msanii mkubwa si masikioni tuu bali hata machoni mwa watu..!

Watanzania pamoja na shida walizo nazo linapokuja swala la kutumia hela kwa burudani huwa wako tayari kabisa tatizo wasanii wetu wanashindwa kutumia fursa..kwakweli Alikiba ni msanii aliye shindwa kuchukua hela ambazo watanzania wanazo kwaajili yake na kipaji alicho nacho!

Nimeamua kuyasema haya kwasababu nimegundua kuna mambo Alikiba na management yake hawaambiwi kabisa na bila shaka wata jitazama upya kama kweli hii ndio thamani ya Alikiba tunaye msikia kila leo!

Karibuni wana jamvi!
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad