Kanisa Langu Halitakufa, Anayetaka Kuliangamiza Ataangamia yeye- Gwajima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema kuna watu wanaotaka kuua kanisa lake lakini kamwe halitakufa na litang’aa hadi katika kizazi cha mwisho.

Akizungumza katika ibada yake iliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema watu hao wamekuwa wakisema kuwa hawalipendi Kanisa la Ufufuo na Uzima na kutaka life.

Alisema kanisa lake lina mamlaka na linaungana na sauti ya damu ya mwana kondoo.

Damu ya Yesu ina sauti kubwa ingawaje ilimwagika miaka mingi iliyopita hivyo watu hao wanapaswa kutambua kuwa wanalindwa na Mungu kwa njia ya damu ya Yesu.

“Hili ni kanisa la Wakristo wa Agano Jipya wasioogopa mambo ya ajabu ajabu na ya upuuzi puuzi na anayetaka kuliangamiza kanisa hili aangamie mwenyewe na ashindwe kwa damu ya Mwanakondoo,” alisema.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alitishia kuzifutia usajili taasisi mbalimbali zikiwamo za dini ambazo alisema zinajihusisha kutoa matamko na kushawishi waumini wao kutekeleza matakwa ya siasa.

Waziri Chikawe alisema atatumia Sheria ya Vyama vya Jamii Sura ya 337 na kanuni zake zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Fungilia mbali watu hawa

    ReplyDelete
  2. KWA KOSA GANI AU UNAROPOKA TU KAMA ZUZU

    ReplyDelete

Top Post Ad