Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Afunguka Kutembea na Mrembo wa Bongo Movies, Kajala Masanja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BAADA ya kuzagaa kwa habari kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ‘kutembea’ na mrembo wa Bongo Movies, Kajala Masanja, mheshimiwa huyo ameibuka na kuzungumzia tuhuma hizo kuwa hazina ukweli wowote zaidi ya kutaka kumchafua katika uongozi wake.

Mapema wiki hii, mitandao mbalimbali ya kijamii ilimtuhumu mheshimiwa huyo kwamba ana uhusiano na muigizaji huyo kwa kudai amekuwa akionekana naye mara kwa mara.Makonda ambaye ameonesha uchapakazi uliotukuka baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa wilaya hiyo mapema mwaka huu, ameweka bayana kuwa kwa muda mrefu kuna watu wenye nia mbaya ambao wanaendesha kampeni ya kumchafua.

“Ni muda mrefu tu, walianza kipindi kile wakati wa Bunge la Katiba nilipokwenda Bungeni na mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, wakasema natembea naye, wakanyamaza. Sasa wamehamia kwa Kajala baada ya kufanya naye kazi.

Hakuna ukweli wowote wanatungatunga tu mambo, watakuwa na sababu zao kwa sababu mtu kama Kajala, maneno yameibuka baada ya kufanya naye project ya kutafuta vipaji vya wasanii.“Nimeshirikiana na wasanii wengi wa kiume katika project hiyo lakini kwa kuwa wameona mwanamke ni Kajala peke yake, wanasema vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Najua kuna wengine wanaoeneza haya mambo wanatumika kisiasa lakini mimi sijali.

Waniache nifanye kazi, najitoa kwa wasanii kwa nia njema ya kutafuta wasanii ambao baadaye wataweza kujitegemea kwani sanaa ni ajira, kamwe hawawezi kurudisha nyuma juhudi zangu,” alisema Makonda ambaye amejiwekea utaratibu wa kukutana na wakazi wake kila Ijumaa kutatua migogoro ya ardhi.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad