Rais Kikwete Apiga Mkwala Asema Hatakubali Misaada Yenye Masharti Kuyumbisha Nchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Jakaya Kikwete amesema nchi yake haitakubali kuyumbishwa na wahisani ambao kila mara wamekuwa wakitishia kusitisha misaada yao kama mambo wanayoyataka yafanywe na serikal hayatafanywa na kuwataka wahisani wenye tabia hiyo kuacha kutumia misaada yao kama fimbo ya kuichapa Tanzania na kama wataendelea kufanya hivyio ipo siku itaikataa hiyo misaada.

Mh Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa mpango wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi yaania Open Govermnent Partineship –OGP ambapo amesema serikali nayo inahadhi yake na siyo kila jambo kuburuzwa.

Kuhusu uendeshaji wa serikali Mh Kikwete amesema wananchi wanapaswa kujua namna shughuli zinavyokwenda ili waweze kuhoji pale mambo yanapokuwa kinyume na matarajio yao.

Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora Mh George Mkuchika amesema tangu Tanzania ingiye katika mpango huo wa OGP mambo mengi ya serikali yamekuwa hadharani na hivyo kuwafanya wananchi wengi kujua namna serikali inavyofanya mambo yake.

Naye mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema jambo muhimu ambalo viongozi wa Afrika wanapaswa kujua ni kwamba wanapaswa kuheshimu utawala wa sheria nakuruhusu uhuru wa mawazo huku akiomba serikali ya Tanzania kuangalia upya sheria yake
ya takwimu na mtandao ili kuweza kutoa fursa kwa watu wengi kutoa mawazo yao.



Chanzo: ITV habari
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAWA MARAISI WA AFRICA AWAPENDI AMBIWA UKWELI AU KUKOSOLEWA, WATU TUNA MATATIZO RUKUKI, NA WANCHI TUKIPINGA WAO HAWATAKI HIYO SHERIA YA SHUT UP ATUITAKI TANZANIA, KWA SABABU UFISADI , WIZI NI MWINGI, MAENDELEO HAKUNA, MADAWA TABU, MAHOSPITALINI WAGONJWA WANALALA, CHINI, SHULE ELIMU DUNI, KILA KTU NI HOVYO HOVYO, NA UKWELI HAWAUTAKI KWA KUWA WAENDELEE NA UOZO WAO, WAO WANAISHI VIZURI NA FAMILIA ZAO, MILO YOTE MARA TATU WANAKULA,HUDUMA NZURI ZA AFYA, SHURE NZURI KWA WATOTO WAO, NA SISI TULIOWAPA MADARAKA TUNANGAIKA, KWA KUWA VYOTE WANAINGIZA MIFUKONI MWAO NA FAMILIA ZAO NA NDUGU JAMAA, NA MARAFIKI, JAMII WALIOBAKI WENGI WANAANGAIKA, ALAFU UKIJA UKWELI OHHH ATUTAKI INGILIWA, NOOO, MBONA SASA SISI KWA SISI TUNAFANYANA WATAWALA WEUSI, TENA AFADHALI YA MTAWALA MWEUPE ANA HURUMA PAMOJA NI MKOLONI ATAWEKA HUDUMA MUHIMU MBELE, KUSHINDA HAWA, ALAFU TUNASEMA TUKO HURU, NA DEMOKRASIA NI USANII TU, HATUKO HURU TUMEJIFUNGA WENYEWE, KWA KUJIAMINI ATI NDUGU YAKO NI MZURI ZAIDI KUMBE NDIO MBWA MWITU

    ReplyDelete

Top Post Ad