Sentensi 18 za Edward Lowassa akitangaza kugombea Urais Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

May 30 2015 inakuwa siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa Tanzania.. bado miezi michache ufanyike uchaguzi mkuu, mmoja ya watu ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo  vya habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid katikati ya Jiji la Arusha ulishuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu ambao walikuja kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia ya kugombea Urais mwaka huu.


  • “Watanzania wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo.. Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. sina shaka tukijipanga vizuri ndani ya CCM tunaweza kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”  Edward Lowassa.
  • “Nchi yetu inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu usioogopa kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. aweze kuwaunganisha Watanzania na kutoa utofauti kati ya walionacho na wasionacho“ Edward Lowassa.
  • “Nina hamu, nina shauku na nina uwezo wa kuiongoza Tanzania… ninaamini nina kila kigezo cha kuibeba dhamana ya nchi yetu.. Katika vitu ninavyojivunia ni pale nilipoenda kupigana vita ya Kagera, nilishiriki kikamilifu nikiwa miongoni mwa askari wa mbele kuikomboa nchi yetu, muwaulize wengine waliwahi hata kufika Kagera?” Edward Lowassa.
  • “Kwa wingi wa rasilimali tulizonazo tuna kila sababu ya kutokuwa ombaomba… Haya ninayoyaeleza ndio msingi wa utendaji wa serikali nitakayoiongoza nikichaguliwa.. nimeamua kugombea Urais ili kupambana na umaskini.. Uongozi wangu utaleta mchakamchaka wa maendeleo” Edward Lowassa.
  • “Najua Watanzania wangapi wanaishi kwa bodaboda, mama ntilie.. hawa ni rafiki zangu hawatafukuzwa barabarani.. ni raia wa Tanzania wanaostahili kula kama wewe“
  • “Kwenye michezo tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu, tutaibadili hali hii kwa kasi sana“  Edward Lowassa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. He leo ndio ameona Tanzania ni ombaomba!!! alikuwa wapi miaka yote hii tangu tumepata uhuru. Hatumtaki nasema hatumtaki fisadi huyu.

    ReplyDelete
  2. Nchi yetu inahitaji viongozi ambao sio wezi, sio wala rushwa, wasiotumia fedha zao kununua wapiga kura kama wewe unavyofanya, sio wabinafsi kila kitu unataka kiwe chako!

    ReplyDelete

Top Post Ad