Wema Sepetu na Idris Nusura Wazichape

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Malkia anayemiliki Kampuni ya Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu na Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15, Idris Sultan ambao wamekuwa marafiki wakubwa katika siku za hivi karibuni, nusu wazichape kavukavu baada ya kupishana kauli huku wivu wa kimapenzi ukitajwa.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar ambapo kwa pamoja walikuwa wamehudhuria sherehe ya utoaji Tuzo za Watu.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tafrani ya wawili hao kutaka kukunjana ilitokea baada ya kumalizika kwa shuguli hiyo ambapo Idris alimpora Wema tuzo yake aliyoshinda na kwenda nayo kwenye gari lake.

Ugomvi huo ulipamba moto na kusababisha watu waliokuwa wakiwashuhudia kutaharuki ambapo Wema alikwenda kwenye gari lake lililokuwa likiendeshwa na Petit Man lakini Idris alimfuata akionekana kumuonea wivu na kumtaka apande gari lake waondoka jambo ambalo Wema alilitolea nje na kumfungia kioo.

Baada ya kuona Wema amemtolea nje, Idris alikwenda kwenye gari lake na kuliegesha mbele ya gari la Wema ‘kum-block’ ili asiondoke ambapo alishuka na kumwambia Petit Man ahakikishe anamfuata kwa nyuma jambo ambalo Petit Man alishindwa kulitekeleza baada ya Wema kukataa.

Baada ya kushuhudia vurugu hizo, mwanahabari wetu alimfuata Wema ili kujua kilichotokea ambapo mwanadada huyo alisema kuwa haelewi ni kitu gani ambacho kilimkuta Idris siku hiyo maana kama angekuwa anakunywa pombe, angesema labda alizidiwa lakini kwa kilichotokea hadi leo hajui ni kipi kilimkuta.

“Yaani hata sielewi Idris alifikwa na nini maana amefanya mambo ya ajabu sana na mara ya kwanza nilijua utani lakini nilimshangaa zaidi baada ya kukomaa hadi kufikia hatua ya kuni-block na gari lake huku akitaka niondoke naye wakati kila mtu alikwenda pale kimpango wake.

“Mimi nadhani kuna utoto fulani bado anao na unamsumbua,” alisema Wema lakini Idris hakupatikana kusema chochote.

Credit: Gpl
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alitaka ukampe utamu

    ReplyDelete
  2. Pesa ya Big Brother inamuwasha

    ReplyDelete
  3. Huwa hamna story za ukweli mpaka muweke za uwongo ndio blog inoge? Hata haipendezi tena kusoma hizi blog zenu heri tusome za Mange anaefanya utafiti kabla ya kuandika au Millard ayo

    ReplyDelete

Top Post Ad