Mpenzi wa Facebook Anayedaiwa Kumnyonga Mke wa Mtu Gesti Huyu Hapa..Siri yafichuka Vidonge vya ARV ndio Chanzo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Charles Raphael anayedaiwa kumnyonga mke wa mtu gesti.
Stori: Makongoro Oging’ na Mayasa Mariwata
MAPYA tena! Yale mauaji ya mke wa mtu, Ashura Maulid yaliyotokea kwa kunyongwa gesti na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa kwenye mtandao wa kijamii Facebook, Charles Raphael (pichani), sasa Uwazi limepata picha yake na mengine yameibuka.


MTUHUMIWA WA MAUAJI
Taarifa kutoka chanzo makini zimeeleza kuwa, mwanaume huyo mpaka anafikwa na tukio hilo la kudaiwa kumuua mwanamke huyo kwa kumnyonga alikuwa akijihusisha na kazi ya ubaharia  kwa safari za ndani na nje ya nchi hasa Yemen ambapo alikuja nchini kuchukua vyeti vyake ili akaajiriwe rasmi nchini huko.

VYANZO VYA POLISI
Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi katika maelezo ya mtuhumiwa huyo, inadaiwa siku ya tukio, wawili hao walikubaliana wakutane kwenye gesti hiyo na kufanya mapenzi.

“Walifanya mapenzi kweli tena bila kinga. Walipomaliza, mwanaume alipekua mkoba wa mwanamke, akakuta vidonge ambavyo yeye alivitafsiri kwamba ni vya kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARV).

MZOZO WAIBUKA
“Mzozo ulianza kuibuka. Mwanaume alimjia juu mwanamke kwamba huenda amemwambukiza virusi vya Ukimwi ingawa mwanamke alijitetea kuwa vidonge vile siyo ARV. “Kwa hasira mwanaume akamshika shingoni na kumkaba, kisha akamwachia na yeye akaondoka,” kilisema chanzo.

Kikaongeza: “Wakati mwanaume anaondoka kwa hasira, mwanamke alikuwa ameanguka chini lakini alikuwa hajafariki dunia. “Ndipo nyuma, wahudumu wa gesti walibaini kuwa, ndani ya chumba hicho kuna mwili wa mwanamke ukiwa chini na kutoa taarifa polisi.”

MTUHUMIWA ALIKAMATWAJE?
Habari zaidi zinadai kuwa, baadhi ya wafanyakazi wenzake marehemu walijua wawili hao walikuwa pamoja kwa hiyo kifo cha mwenzao walikihusisha na mwanaume huyo.

“Ili kumpata mtuhumiwa, polisi walimtumia mfanyakazi mmoja wa marehemu ambaye aliwahi kutongozwa na mwanaume huyo siku za nyuma. Yeye alimpigia simu mwanaume na kumwambia yuko tayari kwa sasa kumpa penzi. Jamaa akafurahi, wakapanga kukutana maeneo ya Jeti, Dar ambapo mtuhumiwa huyo alipofika, polisi walimkamata.

Habari zinasema kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa huku akiwa hajui chochote, akiwa ndani ya gari la kukodi aina ya Toyota Carina (namba zinahifadhiwa) na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar (anakoshikiliwa hadi sasa).

Marehemu Ashura Maulid enzi za uhai wake.

NDANI YA KITUO CHA POLISI
“Alipofikishwa kituoni aliambiwa kuwa ameua mwanamke kwa kumnyonga, akashtuka sana. Akasimuliwa mkasa wote na yeye akajieleza,” kiliongeza chanzo.

POLISI WAVIFANYIA KAZI VIDONGE
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba, polisi walivichukua vidonge hivyo na kuvipeleka kwa wafamasia kwa ukaguzi kama kweli ni ARV lakini vikabainika ni vya minyoo.

MUME WA MAREHEMU
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, siku ya tukio mume wa marehemu, Suleiman Othman alimpigia mkewe simu ili kujua alipo akamwambia anatoka kazini lakini kutokana na foleni za barabarani atachelewa kufika nyumbani.
Taarifa zaidi zinadai kwamba mume alipoona usiku unazidi kuingia, mkewe hajarudi alimpigia simu  ambapo iliita bila kupokelewa baadaye ikawa haipatikani hewani.

TAHADHARI KWA WATUMIA FACEBOOK
Polisi mmoja aliyezungumza na Uwazi kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile siyo msemaji, alisema kumekuwa na kesi nyingi kwenye vituo vya polisi ambapo chanzo chake ni Facebook.“Mimi nawaambia watumiaji wa Facebook kujihadhari na mawasiliano na watu wasiowafahamu, hasa kwenye suala la uhusiano wa mapenzi,” alisema afande huyo.


TUJIKUMBUSHE
Katika gazeti hili toleo lililopita, tuliandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MPENZI WA FACEBOOK AMNNYONGA MKE WA MTU GESTI!
Tukio hilo lilijiri Mei 19, mwaka huu kwenye nyumba ya kulala wageni (guest house) iliyopo maeneo ya Afrikasana, Dar pembezoni mwa barabara ya kwenda Kijitonyama kupitia Polisi Mabatini.

Katika habari hiyo, mume wa marehemu alisema haamini kama mkewe alishawishika kukutana na mwanaume huyo kwa ajili ya kufanya mapenzi tu bali alikuwa na nia ya kumwibia pesa za mauzo ya siku hiyo.Alisema mkewe alikuwa akifanya kazi ya kuuza mafriji kwenye duka moja lililopo maeneo ya Afrikasana, Dar.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acheni kuongopa semeni ukweli jamaa ni seriel killer, inawezekana ndio huyo huyo aliyekuwa anawaua wanawake wengine waliofia Guest Houses kama wale wanafunzi wa Bagamoyo Uni. Amemvunja shingo inavyoonekana wala hakumnyonga kwani walikuta kuna kamba hapo au kitanzi chochote cha kunyongea?

    Ushauri kwa wazazi na walezi na watumiaji wengine wa Facebook, mtu humjui unamuadd wa nini? Utakuta mtu ana marafiki 170 mpaka 1000 kati yao anaowajua labda ni 20 au 30 wengine huwajui wa kazi gani? Na wazazi muwe munamonitor hizo facebook account za watoto wenu.

    ReplyDelete
  2. ni kweli mdau mimi simkubalii mtu friend request kama simjui.nimambo ya ajabu sana unafahamiana na mtu through facebook then mnafikia mahala mnadate bila hata kujua in and out ya huyo mtu.

    ReplyDelete
  3. jamani ni hatare sana watu hawajui tu usimuadd mtu face book kama humjui na huyu jamaa inawezekana kweli ni serial killer.
    watumiaji wa face book jifunzeni kupitia hili.

    ReplyDelete
  4. jaman kujuana sio tatizo tatizo ni akili ya mtu, mimi nina MUME NA WATOTO WAWILI na tulionana fb but mambo yetu yako poa sana si wote wabaya

    ReplyDelete

Top Post Ad