Profesa Tibaijuka Azomewa kwao na Wananchi Mbele ya Kinana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi wa jimbo lake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Hali hiyo ilijitokeza jana asubuhi katika Kata ya Nshamba wilayani hapa wakati msafara wa Kinana ulipofika kuzindua mradi wa maji. Kadhia hiyo ilianza baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Ally Idd Ame kumkaribisha mbunge huyo ili awasalimie wananchi.
 
Hata hivyo, wananchi hao walianza kuzomea kwa zaidi ya sekunde 40 wakipinga Profesa Tibaijuka kupanda jukwaani, hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya, Francis Isack kupanda jukwaani na kutoa kauli ya kiutawala ili kuwanyamazisha wananchi hao.


  • “Anayetaka kusikiliza abaki na asiyetaka aondoke,” alisema Isack na kuwanyamazisha mamia ya wananchi hao. Baada ya kauli hiyo wananchi walitulia na kuruhusu Profesa Tibaijuka kupanda na kuhutubia kwa muda.



  • “Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu, mnaruhusiwa kubadili. Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie aibu mbele ya katibu mkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,” alisema.


Aliwaambia wananchi hao kuwa anachokifanya ni kuwatumikia na kuwaletea maendeleo, hasa wanawake...


  • “Mimi sitafuti kazi na wala sina njaa... na kama hela ya kula ninayo. Mimi sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi mganga njaa muwekeni muone atawasaidia vipi,” alisema.


Akihitimisha salamu zake kwa wananchi hao alisema kama wana jambo lao la ziada walifanye lakini wamuache aendelee na jitihada za kuwaletea wanawake maji... “Sina kinyongo na yeyote kwa sababu “I am too sophisticated (mstaarabu). Nipo juu ya mambo madogomadogo yanayowasumbua.”

Mbunge huyo ambaye hivi karibuni aliondolewa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow, alimweleza Kinana kuwa eneo hilo limekumbwa na upinzani kutoka kwa mtu anayehitaji kulichukua ambaye ni kutoka ndani ya CCM.

Profesa Tibaijuka alisema katika ubunge wake amefufua mradi huo wa maji utakaogharimu Sh200 milioni kupitia shirika moja ambalo mkandarasi wake ni wa Umoja wa Mataifa na utekelezaji umeanza miezi minne iliyopita lakini unahujumiwa.


  • “Mradi huu wa Nshamba unahujumiwa na wapinzani wangu kutoka ndani ya CCM na vyama rafiki vya kisiasa, lakini lengo lao ni kunidhoofisha kisiasa, jambo ambalo linadidimiza maendeleo,” alisema Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN – Habitat).


Kinana na kahawa
Katika ziara hiyo, Kinana aliitaka Serikali mkoani Kagera kusimamia wakulima kuuza kahawa ndani na nje ya nchi ili wanufaike badala ya kuwahusisha na magendo.
 
Kinana alisema wakulima wanahitaji kunufaika na kahawa yao kwa kuwa Serikali haitoi pembejeo kwa zao hilo, hivyo wauze kahawa yao hata kama ni nje ya nchi ilimradi wasivunje sheria

Alisema Serikali haina budi kurekebisha sheria za uzalishaji wa zao la kahawa zilizotungwa enzi za ukoloni inayotaja kuwa mkulima akizalisha zao la biashara linakuwa ni mali ya Serikali, jambo ambalo ni kumnyanyasa.

Alivitaka vyama vya ushirika kuepuka ukiritimba wa kutoa bei ndogo ya mazao ya wakulima na kutaka wanapowachagua viongozi wa ushirika, waangalie walio na uadilifu katika matumizi ya fedha.

Fedha za Mwenge
Akiwa katika visiwa vya Bumbire na Mazinga, Kinana aliitaka Serikali kusitisha uchangishaji wa fedha za Mwenge ambao hautawafikia wananchi, akisema kitendo hicho ni kuwanyanyasa na kuwadhulumu.


  • “Uchangiaji wa mafuta ya Mwenge ni wa hiari, si  kuwalazimisha wananchi na kusababisha Serikali kutoaminiwa na mkichangisha fedha hakikisha Mwenge huo unafika kwa wananchi wa eneo husika,” alisema Kinana.


Aliitaka Serikali ihakikishe inawalipa posho askari wake wanaoimarisha ulinzi na usalama majini na nchi kavu badala ya kuwatoza fedha wananchi kuchangia vyombo hivyo vinapokuwa vikitimiza majukumu ya kiserikali visiwani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mama Tibaijuka anaonyesha dharau na jeuri ya fedha za wizi! Hongereni sana wananchi mliomzomea mmeonyesha upeo na upevu wa akili. Anaiba fedha zetu waganga njaa na bila aibu wala adabu anajaribu kututukana. Ushauri wa bure mama ni kwamba malipo siku hizi ni hapahapa duniani utaendelea kupokea mapigo hadi unyooke. Na hutakaa upate amani ya rohoni. Kuhusu siasa sahau tena mama (o) (o) (o) (o). Ulijigamba kua wewe ni Jembe la Kikwete akakuchinjia baharini. Sasa sijui utajiganba tena wewe kua ni jembe la Ban Ki-moon???? :>) :>) :>) Hiyo ndo shida ya uongozi wa chupi.........unavuliwa chupi unagawiwa uongozi.Wananchi tuamke

    ReplyDelete
  2. Sasa wanapanda jukwani nakutumia kauli za nguvu anaetaka aondoke asietaka abaki, wanachi wangekuwa na umoja wote wangeondoka na kuwacha wao pekee yao, kwanza hawana hata la maana zaidi zidi tu ya kupanda majukwani na kuwadanganya wanachi wamesha wachoka, kuwajibika hawajui, bali wanapenda nyenyekewa, u niggers u dictater and poison

    ReplyDelete
  3. Kikwete Hajamvua Chupi bwana, Mbona Maza Mwenyewe Sura Ngumu Kama nini , Presidaa wetu ana Taste ya Vimwana Warembo Like Salma K. Huyo Maza ni Mburula hata mimi ningemzomea tena hapo ningesepa kabisaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad