AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa katika mahojiano maalum wikiendi iliyopita, TID ambaye ni mmiliki wa Top Band alifunguka kuwa miongoni mwa mambo yanayomkosesha raha na amani ya moyo, ni pamoja na kuhukumiwa kujihusisha na matumizi ya unga na wengine kwenda mbele kwa kusema hata kushuka kwake kisanii kumechangiwa na ishu hiyo.
Staa huyo wa Ngoma ya Kiuno alisema kuwa, wakati mwingine watu wanamsakama hadi mama yake mzazi wakimtaka amkanye mwanaye kujiepusha na maisha ya ‘kubwia unga’ jambo ambalo linampa wakati mgumu na kujiona kuonewa katika jamii.
Kuhusu kushuka kimuziki, TID alisema miongoni mwa sababu zilizosababisha kuporomoka katika anga la muziki ni kile alichokiita ‘hujuma’ kutoka kwa baadhi ya wadau wakubwa wa muziki (majina yapo), kwa kushindwa kumpa fursa za kimuziki zikiwemo promosheni na mialiko ya shoo kwa kuwa wana vinyongo na fitina dhidi yake.
“Kaka, naonewa kabisa nikihusishwa natumia madawa ya kulevya, wanamsumbua mama eti akae na mimi anionye.
“Jamani situmii madawa ya kulevya kama cocaine, ila kwa upande wa bangi ni sawa nakubali kuwa navuta.
“Lakini pia, kuvuta kwangu bangi siyo sababu ya mimi kushuka kisanii, zipo sababu zingine kabisa kama kuhujumiwa na wadau wakubwa wa soko la muziki kutokana na mabifu yanayotokana na sababu binafsi.
“Hivi kweli mtu anayetumia madawa ya kulevya kama cocaine, anaweza kumudu maisha kama kununua nyumba? Kununua magari? Hata kuendelea kuimba kweli? Siyo sawa jamani,” alisema TID.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
lakini bangi haibadilishi mtu kiasi alivyobadilika TID.labda bangi hiyo ni aina pekee.
ReplyDeletebob Marley alikuwa anaitumia sana .lakini hakuisha wala hakubadilika kiafya kama TID.UTAAMINI Anavyojitetea?