safari Hii Nampa Kura Yangu Fisadi.............

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jamani nimechoka, mwaka 1995 nilitapeliwa, niliuziwa mbuzi kwenye gunia baada ya kuletewa mmachinga mmoja nikaambiwa ni mr. clean na bila hiana nikatoa kura yangu. Matokeo, amekaa ikulu miaka 10 akaua viwanda vyangu, akauza benki yangu ya taifa na akafungua ya kwake, akaua shirika langu la bima ili afungue la kwake, akafungua kampuni kwa anuani ya ikulu na kujimilikisha migodi yangu mimi mpiga kura, akawa na kiburi cha ajabu na kuanza kuniita mchwara, akauza nyumba zangu zote akishirikiana na ma-padlocks. Siku hizi anatembelea magari ya tinted ili asizomewe kwa jinsi alivyochafuka, sasa eti amesafiri hadi Chato kumuibua another mr clean kama yeye! Sikubali.

Ok hayo yakapita ikaja 2005, nikaletewa malaika mwenye sura nzuri kutoka Msoga hana kitu chochote zaidi ya sura yenye mvuto. Akaja na ahadi kemkem za maisha bora kwa kila mtanzania lakini baada ya miaka mingine 10, amefanikiwa kutimiza hiyo ahadi kwa familia yake tu, taifa zima bado tunasubiria hizo ahadi. Tumeshuhudia mambo ya ajabu kama escrow, utapeli kwenye bomba la gesi na mikataba ya kuchimba madini, gesi, nk.

Safari hii sifanganyiki, hawa ninaoletewa wanaoitwa wasafi halafu nikishawapa kura yangu wananiliza, wanasema kwamba kwa miaka yote 10 waliwasahau wazazi wangu wakulima, wanachomoka na mali zangu mimi mpiga kura, halafu hawataki hata niwaulize chochote.

Safari hii nimebadilisha mawazo. NAMCHAGUA FISADI maana yeye sitamshangaa akiniibia maana mmeshasema kwamba ni fisadi. Naumia sana ninaposhawishiwa kumchagua "msafi" halafu ananiibia. SAFARI HII SIDANGANYIKI, NAMCHAGUA FISADI.

By Mwananchit/JF
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. umenena!!!ni bora fisadi ambaye alijitoa ili baba asivuliwe nguo

    ReplyDelete

Top Post Ad