Wakongwe Wenzangu Wengi Wamepigwa KO Kimuziki, Mimi Nadunda Bado – Dully Sykes

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kama ingekuwa masumbwi, Dully Sykes anadai wasanii wakongwe wenzake wengi wamepigwa kwa Knock Out, lakini yeye bado anadunda tu.

Dully ameiambia Bongo5 kuwa hiyo ndio tofauti kubwa aliyonayo dhidi ya wenzake.

“Mimi ni tofauti na wasanii wote, mimi ni msanii nisiyetabirika, mimi ni bondia ambaye napigwa lakini sipigwi kwa Knock Out, mimi sipigwi kwa KO hata siku moja, mimi nitapigwa tu kwa point,” amejinadi Dully.

“Kwahiyo point ni kitu cha kujifunza hapa nimekosea wapi na nijirekebishe vipi ambapo ni tofauti na wasanii wenzangu wa zamani ambao tayari wameshapigwa kwa KO. Sasa hivi siwaoni na siwasikii, lakini ukiuliza Dully Sykes bado nipo. Unajua kuna wasanii wengine wanakuwa wanachanganyikiwa wanaingia kwenye madawa kwa sababu wanakuwa hawakubali ile hali. Mimi nakubali na najua kabisa kuna mchana na usiku. Kama wako ulikuwa ni mchana unapoingia usiku pumzika subiria mchana wako. Mimi nawashukuru mashabiki wangu kwa kuendekea kunisupport na kuendelea kunipenda mpaka leo hii na kunipa nafasi ya kuonekana kama msanii mpya yaani upcoming,” ameongeza Dully.

Kwa upande mwingine Dully amekiri kuwa video ya wimbo wake Shuka imegoma. Amesema muziki wa sasa umejaa changamoto nyingi hivyo kila msanii anahitaji kuwa mvumilivu katika wakati kama huu na kukubali matokeo.

“Mpaka sasa hivi rotation ya video haina nguvu lakini audio inafanya vizuri. Unajua sio kila kitu unachotoa kinaweza kuwa bora. Kuna wasanii ambao sasa hivi ndo wanafanya vizuri na pia wanatoa ngoma zinagoma. Hii ni hali ya kila msanii, inafikia wakati sio kila kitu kinaweza kufanikisha. Kwa sababu kuna nyimbo nyingi za wasanii wazuri na zinagoma na pia ninaamini sio kila siku nitakuwa Dully Sykes, wakati kila siku kuna wasanii wapya wanakuja na wanafanya vizuri. Kwahiyo lazima tupeane nafasi. Hivi vitu vipo tangia zamani na kila kitu lazima kiwe na wakati.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad