Chadema, CCM Vita Kali..Wachuana Vikali Matangazo ya Televisheni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vyama vya Chadema na CCM vimeingia katika mchuano wa kuwania nafasi ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya kampeni za wagombea urais katika televisheni Jumamosi hii.
Wakati Chadema ikitaka muda wa kurusha matangazo ya uzinduzi wa kampeni za mgombea wake, Edward Lowassa kutokea jijini Dar es Salaam, CCM inataka kurusha matangazo ya mkutano wa kampeni ya mgombea wake, Dk John Magufuli kutoka jijini Mbeya.

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa kumekuwa na njama za CCM kutaka kuzuia fursa ya Chadema kurusha kampeni za mgombea wake kwa kutaka siku hiyo irushe kampeni za Dk Magufuli.

Akizungumzia madai hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikiri chama hicho kutaka kurusha matangazo ya mgombea wake na kuhoji; “tatizo liko wapi kama Chadema imechelewa kulipia?”

Ni kweli mgombea wetu wa urais akiwa Mbeya tutarusha matangazo ya kampeni zake moja kwa moja kwenye runinga, sasa ni runinga ngapi siwezi kujua maana kuna watu wanalifanyika kazi suala hilo. Lakini kama Chadema walijua wana tukio lao kwa nini wasingewahi kulipia?” alihoji.
Chanzo cha habari kutoka kituo kimoja maarufu, kimeeleza kuwa kwa nyakati tofauti, CCM na Chadema waliomba muda wa kurusha vipindi vyao, lakini CCM ndiyo waliofanikiwa kupata.
Ninachojua hao wote walikuja kwa nyakati tofauti kuomba muda na CCM ndiyo waliofanikiwa kupata,” alidokeza mmoja wa wafanyakazi wa telesheni hiyo ambaye hakutaka kutaja jina kwa maelezo kuwa siyo msemaji.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam TV, Tido Mhando alisema CCM na Chadema vilikuwa vimeomba kurushiwa matangazo yao na vyote vimelipia. Alisema kila moja kitapata fursa hiyo kwa kuwa kituo chake kina channel nyingi.

Hata hivyo, mmoja wa wahariri wa Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1), alisema: “Sisi tunarusha vipindi vyetu kulingana na matukio na mahitaji ya jamii, hatuko fixed.” Alieleza kuwa ameamua kutoa jibu hilo rahisi kwa kuwa alijua kwa nini mwandishi aliuliza.

Sisi hatuna utaratibu wa kurusha live (moja kwa moja), wanaofanya hivyo ni watu wa radio tena huwa hilo linafanywa kibiashara. Kwamba wateja wanaomba kutangaziwa vipindi vyao na kulipa fedha,” kilieleza chanzo kutoka kituo kingine.

Habari zimeeleza kuwa kituo kimoja kikubwa cha televisheni kimethibitisha kurusha matangazo ya mgombea wa Chadema.
Awali, Makene alisema hadi jana, chama hicho kilikuwa kimefanikiwa kupata vituo vinne na radio nne.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna watu respectable wenye CV zao za maana duniani…lakini walivyojihusisha na CCM wamechafua CV zao;
    Mfano;
    Getruda Mongela mwanamama aiyeongoza mkutano wa Beijing unajua kashfa za rushwa zilizokuja kumkumba
    Sospeter Muhongo-A respectable Journalist unajua Amefanya nini kwenye ESCROW
    Omar Nundu mtaalamu wa dunia wa usafiri wa anga unajua ni nini kimemtokea
    Prof Anna Tibaijuka mama aliyeongoza shirika la Umoja wa mataifa unajua nini kimemtokea
    Daudi Balali a respectable IMF and World Bank Economist unajua nini kimemtokea baada ya kujihusisha na CCM.
    Ukiachana na hao…Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani alikuwa mtu mchapa kazi…Katika wizara alizopita kabla ya hapo alikuwa mwadilifu na Mchapa kazi…alichaguliwa kwa 80% kumbuka….Nini kimetokea baada ya kuwa Ikulu?
    Benjamin Mkapa..Jembe la Nyerere aliingia kama mzee wa kazi ameondoka na kujimilikisha mgodi wa Kiwira.
    Magufuli anayegombea urais wa CCM Alishiriki kikamilifu katika kuuza nyumba za serikali….Ameshiriki kuiingiza hasara serikali majuzi kwenye kivuko ca kigamboni shs Bilioni 8…Kivuko hakina muda wa miezi mitano lakini hakifanyi kazi ….ameiingiza hasara serikali kwa maamuzi mabovu mengi aliyofanya.
    Ndio maana kwa tunaotazama mambo kwa umbali ni bora CCM ikakaa pembeni tuanze upya (Sio kwamba wapinzani ni wazuri sana)…Kutakuwa na maumivu ya miaka 5 lakini baada ya hapo tuta endelea kama taifa.
    Kama taifa inabidi tuweze kufanya maamuzi magumu kwa mustakabali wa vizazi vyetu vijavyo.
    Mfano kulikua na haja gani ya kumilikisha kampuni za wazungu gesi yetu kwa miaka 99…tena kwa mikataba ya siri…….
    Utakuwa kichaa kudahani magufuli ataipitia hio mikataba na kuifumua…You must be mad

    ReplyDelete
  2. Nape, wacha upumbavu na ulofa aliosema babako chinga nkapa

    ReplyDelete
  3. CCM KIMSINGI NA KWA MANTIKI YA MFUMO HALALI WA DEMOKRASIA YA USTAARABU HAITOKUBALI KUSHUHUDIA KUANGUSHWA VIBAYA HIVI KAMA INAVYOJIDHIHIRISHA NA MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA.WAINGEREZA WANASEMA FIGHTING TO LOSE THE LAST BATTON YAANI ANGUKO LA MWISHO WA UHAI WAO WA UTAWALA WA MIAKA 55 JAMANI KUTAWALA KUNA DARAJA LAKE TENA KUU SANA.WANATUPIA SASA TUNASHUHUDIA MAWE FIMBO KUNI KOKOLO SOCKS UNDERWEAR KIATU CHA KIKWETE KOTI OVERSIZE LA MKAPA MASHINE YA NDEVU YA MAGUFULI YOOOOTE HAYO ILI MRADI WAJINASUE HANUSURIKI MTU HAPA FANYENI KILA AINA YA HILA NA VITIMBI AMBAVYO TAYARI TUMESHAANZA KUANDAA VITABU JUU YA ANGUKO LAO.HAPA WANAPASWA KUELEWA KWAMBA TULIKWISHA AMUA KUA RAIS WA TANZANIA WA AWAMU YA TANO NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA HATA BILA YA KUSUBIRIA KAMPENI YAKE KWETU ASIONGEE LOLOTE APUNGE TUU MKONO.ATAONGEA SIKU YA KUAPISHWA TAREHE 30 OCTOBA 2015.MUACHE MDOMO WA CHURA APULIZE ZUMARI

    ReplyDelete

Top Post Ad