Zitto Kabwe Asema Magufuli ni FISADI.......Awaponda UKAWA Kumteua Lowassa Kuwa Mgombea Urais Kwa Kuwa naye ni FISADI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli  si msafi katika utendaji kazi wake kama inavyoelezwa kwa Watanzania.

Moja ya kigezo kinachotumiwa na Zitto ni madai ya ‘kukwapuliwa’ kwa Sh. bilioni 87 za Wizara ya Ujenzi anayoongoza.

Alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh. bilioni 252 za miradi ya umeme, barabara na miradi maalumu zilizokosa maelezo yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali aliyowahi kuiongoza akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Zitto alisema kukosekana kwa fedha hizo ni kiashiria cha kuwapo matumizi mabaya katika wizara iliyoongozwa na Magufuli.

Awaponda  UKAWA.
Zitto alivibeza vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa vimepoteza dira baada ya kumpokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kutoka CCM na kumteua kuwa mgombea urais wao.

Alisema Zitto alipinga hoja iliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wa Ukawa kuhusu ufisadi kuwa ni mfumo na si mtu binafsi.

Zitto alisema ACT-Wazalendo inalenga kujenga siasa mpya nchini zinazojielekeza katika utii wa maadili na kiongozi wa umma kutangaza mali zake hadharani.

Alitoa wito kwa wapiga kura kuwachagua wagombea wa chama hicho kwa madai kuwa vyama vinavyounda Ukawa vina taswira isiyotofautiana na CCM.

Naye Mweyekiti wa chama hicho, Anna Mughwira, alisema chama chake kitakapompitisha rasmi kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Singida Mjini, ataelezea namna atakavyofanikisha kuleta mabadiliko na kuharakisha maendeleo.

“Singida iliachwa nyuma kwa maendeleo tangu enzi ya mkoloni…sasa ni lazima tubadilike ili tupate maendeleo,” alisema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ACT MMEISHIWA MANENO MAPEMAAAA! SEMA SERA ZA CHAMA CHAKO ACHANA NA UFISADI MBONA HATA WEWE NI FISADI? UTAJIKUTA HATA MBUNGE 1 HUNA KWA AJILI YA KELELE ZAKO

    ReplyDelete
  2. Kila mmoja atasema kumpembua mwenzie kutetea tumbo lake hakuna lolote la maana hizi siasa za kizamani ktk dunia yetu ya leo kwa nini wabongo bado twaburuzwa na bakora tunayo wenyewe ktk masanduku ya kura ingekuwa tunaitumia vizuri tunawaadibisha hawa wanasiasa wetu kupitia njia hio ya kura wangekoma kutufanya wajinga wangeshika adabu na kuzungumzia yaliyo na maana na kuwajibika kwa heshima na adabu wengi wa wanasiasa wetu ni njaa tupu akitumuliwa huku anakimbilia kule ndo biashara zao

    ReplyDelete
  3. Zito alikula ela escrow toka kwa Seth

    ReplyDelete
  4. ZITTO HANA SERA ZAIDI YA KUKOSOA CHADEMA

    ReplyDelete

Top Post Ad