Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba Akana Kujiuzulu Uenyekiti CUF

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia kutokea sintofahamu iliyopelekea mkutano wa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Waandishi wa  Habari  kuahirishwa jana  asubuhi hatimaye, mida  ya  saa  nane  mchana  Prof. Lipumba alijitokeza na kukana kujiulu.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuanzia juzi zilienea taarifa kuwa Prof. Lipumba amejiuzulu, suala lililopelekea jana kuitishwa mkutano na Waandishi wa Habari katika ofisi zao zilizopo Buguruni jijini Dar es salaam lakini  ghafla mkutano huo uliahirishwa.

Sababu ya kuahirishwa mkutano huo inadaiwa kuwa  ni wazee wa  chama  hicho kumtaka Prof. Lipumba kuwaeleza kile alichopanga kuzungumza na waandishi .

Wazee kadhaa walichaguana na kwenda kuonana naye kujua alichokuwa amekusudia kuzungumza na waandishi wa habari hasa baada ya kuwapo kwa tetesi za kutaka kujiuzulu.

Akizungumza mara baada ya kufanya kikao na wazee hao Prof. Lipumba alisema kuwa hajajiuzulu  na kuwataka wanachama   kuhakikisha   kuwa  wanakijenga  chama  cha CUF.

“Mwaka 1995 nilikuwa mwanachama wa kawaida nilipogombea urais kwa tiketi ya CUF na mwaka 1999 nilikuwa mwanachama wa kawaida nilipoongoza kampeni za Jimbo la Temeke na Ubungo ambapo tulishinda lakini wakatuibia kura.

“Chama ni taasisi na tukijenge kama taasisi, ni wajibu wa kila mwanachama bila kujali nafasi aliyonayo kukijenga,” alisema na kuhitimisha kwa salamu ya; “hakiii” na kujibiwa “kwa wote,”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad