Mwigizaji Lulu Michael, Mama Kanumba Wapigana Vikumbo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAKUBWA! Mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amejikuta kwenye simanzi nzito baada ya kukutana na mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alikuwa mpenzi wa mwanaye kumpita bila kumsalimia.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar kulipokuwa na fainali za shindano la vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) ambapo Lulu alimpita mama huyo kama hawajuani kitendo ambacho kilisababisha minong’ono ukumbini hapo.
FrolaMtegoa“Inastaajabisha sana yaani huyu Lulu ndiyo kafikia hatua ya kumdharau mama Kanumba kiasi hiki, siyo siri hamtendei haki huyu mama sijui ni kitu gani kikubwa ambacho alimkosea,” alisikika mmoja wa mashabiki.

Mama Kanumba alipohojiwa na paparazi wetu ukumbini hapo, alisema anashindwa kumuelewa Lulu kwani hata ukiondoa undugu wake, bado kiumri ni mtoto anayepaswa kuheshimu wakubwa.
“Nimestaajabu sana kuona Lulu hanisalimii na isitoshe alijifanya kama hana habari na mimi utasema kuna kitu nimemkosea, wakati yeye ndiye anatakiwa ajishushe kutokana na yale yaliyotokea, ni dharau kubwa amenionyesha wakati aliwahi kuniomba msamaha huko nyuma kuhusu matukio yake hayahaya ya kuninunia,” alisema mama Kanumba.

Alipotafutwa Lulu, simu yake haikuwa hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

Source:Globalpublishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Oops jamani
    Lulu alikuwa ex wa kanumba
    Mama kanumba usimzibie riski Lulu
    Mtu mzima ovyo
    Lulu she is still young and sexy
    Usiingize u bi mkora kwenye maisha ta Lulu
    Na kama u ataka chat au palata au kimango
    Mtumie Lulu
    Fanya movie na yeye
    Lakini bla bla Kama kunguru weusi hutapata
    Lulu anauzika ongea naye Kama msanii
    Usimwendee kwa gia ya kanumba

    ReplyDelete

Top Post Ad