Nikiwa Mbunge Msinitegemee Sana Kuongelea Matatizo ya Wasanii – Professor Jay

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wasanii wasitegemee msaada wa maana pindi Professor Jay akiingia bungeni. Rapper huyo anayewania ubunge kwenye jimbo la Mikumi mkoani Morogoro amesema atatumia wadhifa huo kuwahudumia wananchi wa Mikumi.

Professor amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi hivyo atatumia muda kuwatumikia watu wake.

“Nimewaambia wasanii wangu na wanajua nimechaguliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye jimbo la Mikumi, lakini wengi wamesema watanisaidia kwa maneno lakini bado sijalaunch kampeni yangu rasmi. Natarajia kulaunch natarajia rasmi tarehe 5 mwezi wa tisa, sasa tunaangalia nani atani-support,” amesema.

“Mimi ni kijana na mimi ni mwanamuziki, watu waelewe naingia bungeni kwenda kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Mikumi, kwahiyo tutafanya kazi sawa za wananchi wa jimbo la Mikumi na Professor atakuwa anaishi Mikumi na nitakuwa napatikana huko Mikumi.”

“Watu wasitegemee nitaingia bungeni kwenda kuongea masuala ya wasanii sana kuliko hata kuwawakilisha watu wa Mikumi. Watu wajue Professor Jay atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi ni vile ni mwanamuziki nitapigania kwa hali na mali maslahi ya muziki ili kuweka sanaa katika level za juu zaidi.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. prof jay kufanya siasa pamoja na akina Sugu na Afande sele wakati ni wasanii vioo vya jamii si tatizo, lakini DIAMOND kuonyesha mapenzi yake kwa CCM ni tatizo

    ReplyDelete
  2. prof jay kufanya siasa pamoja na akina Sugu na Afande sele wakati ni wasanii vioo vya jamii si tatizo, lakini DIAMOND kuonyesha mapenzi yake kwa CCM ni tatizo

    ReplyDelete
  3. Mtize umesema kweli hao wakina profesa Jay kwa vile ukawa nijambo la kawaida kwa hao wanao jiita watanzania wanashangaza sana na hapa wamepita kimya hakuna aliye weka coment kila mtu anahaki ya kukipenda chama chake bila kutukanwa wa Tanzania tubadilike.

    ReplyDelete
  4. Bila kufanya music hata hao wa mikumi wasinge kujua, lzm uwatete wanamuziki coz ndio unaokupeleka bungeni

    ReplyDelete

Top Post Ad