UKAWA Mnaniharibia Mwanangu, Nakosa Raha Nyumbani Kwangu Mwenyewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kila nikitaka kwenda nyumbani kwangu,nasitasita. Natafakari namna na kujibu mapigo ya mpigo toka kwa mwanangu. Kijana wangu huyu aliye Chuo Kikuu,akiwa likizoni sasa,ananitambia na kunibeza katika nyumba yangu mwenyewe.

Najuta kumpa uhuru wa kidemokrasia tangu akiwa Shule ya Msingi. Kila akiniona ananitambia kuhusu UKAWA na kukwama kwetu kama CCM.

Nimejaribu kumwambia kuwa mimi sipo tena kwenye kampeni za CCM. Bado ananing'ang'ania. Ananibakisha CCM na kunihusisha moja kwa moja na kampeni za wagombea wetu kuanzia Dr.Magufuli, Mama Samia, wale wa Ubunge na Udiwani.

Nyumba yangu mwenyewe imegeuka uwanja wa tambo na vikumbo vya kikampeni. Yeye amejipambanua kuwa ni mfuasi wa UKAWA kupitia CHADEMA.

Leo, ameshanipigia simu kujiproud kuwa Lowassa anaibomoa ngome ya CCM pale Millenium Towers. Anadai kuwa Lowassa atawateka wanawake wa Tanzania na kuifanya CCM ibaki na wazee tu kama wapigakura wake.

Akajinasibu kuwa wanawake wa Tanzania wanaiacha mkono CCM na inaelekea kuyumba pamoja ya karata yake ya kumsimamisha Mama Samia kama mgombea mwenza.

Leo pia, amenidokeza kuwa watanzania hawa si wale. Amesema kuwa ana tafiti zilizo fiti zikionesha kuwa UKAWA ndiyo dawa. Ananisubiri anioneshe nikifika nyumbani jioni.

Lengo lake nalijua. Ni kuninyanyasa kisiasa lakini kisasa. Kwa hoja za haja bila kubadili lahaja. Najiandaa,kwa kujisomea nyaraka za haraka na baraka,kwenda kupindua tafiti zake. Nikifika nyumbani, kampeni za chumba kwa chumba zitaanza.

UKAWA mmeniharibia mwanangu. Kwasasa hadi ana kibwagizo chake: MAGUFULI APIGE KAMPENI, LOWASSA ATAPIGIWA KURA! Kazi kwelikweli.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. POLE SANA MZEE MWENZANGU YAMEKUKUTA YANAYOENDELEA KUKUKUTA.NI WIMBI KUU LA MABADIRIKO AMBAYO HAYAJAWAHI KUONEKANA TANGU TUPATE UHURU.CCM INAMFIA KIKWETE MIKONONI MWAKE NAOMBA NIELEWEKE CCM KUFA NI KULE KUTUNGULIWA KUTOKA KUSHIKA HATAMU ZA DOLA HADI KUWA CHAMA CHA UPINZANI POTELEA KIWE NA WABUNGE 100 BUNGENI NI SAWA NA BURE TUU.KUKOSA KUTAWALA NCHI LITAKUA PIGO KULIKO MAPIGO YOTE.UCHUNGU WA MOYO UTAKUA HAUNA KIPIMO MAGOMVI NDANI YA CHAMA HAMAHAMA KUPINDULIWA UONGOZI NA WANACHAMA NGUMI MAKUNDI KUFUKUZANA KABALI MATUSI KUIBUKA VYAMA VIPYA NDANI YA CHAMA[OFFSHOOTS] KUFUNGLIANA KESI NA MENGI MENGINEYO.NASEMA HIVI MZEE TUOMBE UHAI KAMA MIMI MUONGO TUOMBE UHAI.MWISHO NAOMBA NIKUUDHI MZEE KWA KUKUPA NENO LILILO MOYONI MWANGU NALO NI HILI;MHESHIMIWA LOWASSA SAMBARAISHA HAWA PIMBI KOMBAMWITU CCM WAANGUSHIE LAANA KUU KUTOKANA NA WIZI WAO MKUBWA WAMEIFILISI NCHI WAMEUANGUSHA UCHUMI WETU,WALIONE JUA LIKITUA TUU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Rowassa kabadili jezi naye ni fisad vile vile

      Delete
  2. Asante anyonimous 27 octoba 2015 at 6;31pm kwa ujumbe wako mzito wenye picha kamili ya kilichopo kwa sasa kinachotegemewa kutokea katika siasa kuu za nchi yetu.japo mlengwa wako alikua ni mzee anayesononeka kwamba sasa hivi binti yake msomi kwa sasa ni ukawa kupindukia na kwamba binti huyo kwa sasa maisha yake kwa hali na mali ni LOWASSA MABADIRIKO NA MABADIRIKO LOWASSA.ujumbe ule mzito naomba uchukuliwe uzito wa pekee uhifadhiwe mioyoni mwetu wapenda maendeleo watanzania woote wenye akili timamu.waachiwe wenye akili ngumu kufunguka na kukubali ukweli waendelee kubakia chama tarajiwa cha upinzani LOWASSA YUPO KWA AJILI YAKO LOWASSA YUPO KWA AJILI YANGU LOWASSA YUPO KWA AJILI YETU WOOOTE.Mlio na hofu bado kumbukeni hizo si hofu halali bali ni hofu zinazotawaliwa na MAPEPO MACHAFU na mnastahili kuombewa kwa nguvu zoe.MUNGU IBARIKI ANZANIA MUNGU UBARIKI UCHAGUZI WETU MKUU MUNGU UMBARIKIE RAIS WEU MTARAJIWA MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA ATUTAWALE KWA AMANI UTULIVU NA HEKIMA KUBWA.KWA JICHO LA HURUMA ATUANGALIE SISI MASKINI MALOFA.

    ReplyDelete

Top Post Ad