Updates: Mkutano wa Edward Lowassa na wanawake wa DSM kutoka Ukumbi wa Millenium Tower

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kama tulivyowatangazia jana rais matarajiwa wa awamu ya tano Kamanda mpambanaji asiyechoka na mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa atalihutubia Taifa kupitia wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kusikiliza kilio cha wanawake wa Tanzania na atatoa mwelekeo wa UKAWA kwa wanawake na Taifa kwa ujumla baada ya kushika dola mwezi Oktoba.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi saa 8 mchana na utarushwa moja kwa moja na kituo bora cha Televsheni Tanzania cha ITV.

Kati ya wanaotarajiwa kuhudhuria ni wanawake wajasiriamali,mama ntilie,wafanya usafi,akina mama wa nyumbani,wanaoishi katika mazingira magumu,wenye ulemavu na waliojariwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Mgombea huyo wa Urais kupitia UKAWA atakutana na wanawake hao ikiwa ni siku moja tangu serikali ya CCM kumpiga marufuku kukutana na wafanyabiahsra mbalimbali masokoni,wagonjwa mahospitalini na pia kumzuia kupanda daladala.

Wakati Lowassa akitendewa hayo mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu amekuwa akisindikizwa na polisi kutembelea wagonjwa mahospitalini na ni juzi tu alikuwa katika hospitali ya HUruma Mkuu Rombo ambapo alikutana na wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo na kusababisha shughuli katika hospitali hiyo kusimama kwa zaidi ya saa tatu.

Timu ya wanahabari wa UKAWA imeshafika hapa Ukumbini na tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri kabla na wakati wa mkutano.

Karibuni..
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. EWE MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MJALIE MJA WAKO MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA AFYA NJEMA UJASIRI MKUBWA UIMARA ZAIDI WA ROHO NA MOYO EWE MOLA WETU ALAH KARIM KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU KWAKE NA KWETU SOTE WATANZANIA TUNAPOKWAZWA NA MAKUSUDI SHETUWAN YA CCM NA VYOMBO VYAKE VYA DOLA ILI MOLA WETU IFIKE 25 octoba TAREHE TUMPE KURA ZETU ZOOTE ZA NDIO AAPISHWE SALAMA KUSHIKA DOLA NA AANZE RASMI KAZI YAKE YA KUTUTUMIKIA MALOFA

    ReplyDelete

Top Post Ad