Kajala Masanja Anatoa Wapi Jeuri Hii ya Fedha....?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Imelda mtema
FEDHA inaongea! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji Kajala Masanja kupanga kwenye mjengo mpya wa maana na kuushehenesha samani na ‘vikorombwezo’ kibao hadi kufikia hatua ya watu kuhoji, amepata wapi jeuri hiyo ya fedha? Ijumaa limenasa mchapo kamili.
Mjengo anaoishi mwigizaji Kajala Masanja.
Kajala ambaye awali alikuwa akiishi maeneo ya Sinza-Madukani, kwa sasa amehamia katika mjengo huo mpya uliopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo, ndani ya mjengo huo, Kajala anaishi na mwanaye Paula huku akiwa amewaajiri wafanyakazi wa ndani watatu na kulindwa na kampuni maalum ya ulinzi.
“Yani Kajala ananuka hela. Mjengo wake mpya una kila kitu ndani. Ukiingia unaweza kupagawa kutokana na vitu vilivyomo ndani. Watu tunajiuliza ni nani anayempa jeuri hii maana filamu pekee haziwezi kufanya matusi haya,” kilisema chanzo hicho.
...Sebuleni.
Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alitia timu nyumbani hapo kwa Kajala na kujionea nyumba hiyo ya kifahari aliyopanga sambamba na ‘mazagazaga’ kibao ya thamani yaliyomo ndani.
Alipoulizwa amepata wapi jeuri ya kupanga nyumba hiyo ya gharama ambayo hakutaka kutaja bei ya kodi, kuajiri wafanyakazi watatu na kampuni ya ulinzi, Kajala alidai mambo yote hayo ameyafanikisha kwa kazi ya mikono yake na si vinginevyo.
“Unajua kuna kipindi cha nyuma nilitengeneza filamu zangu kama tano na nilikuwa na maana hata kama nisingepata zile hela kwa wakati ule lakini nilijua baadaye nitapata hela nzuri na nitatengeneza maisha yangu hivyo sasa ndiyo nimevuna matunda ya sinema hizo na kufanya haya unayoyaona,” alisema Kajala licha ya nyuma ya pazia kuwepo na madai kuwa kuna kigogo anamuweka mjini.
Source:GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hiyo nyumba amepanga au ameinunua?? Kama amepanga, hiyo pesa anayolipa kama kodi isingetosha kujenga nyumba yake mwenyewe?? Nyinyi waandishi wa habari ndio mnaowaharibu hawa wasanii, mnamsifia mtu kwa kupanga nyumba?? kweli?? Msifie mtu kama amejenga ya kwake...okay

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeongea point. mwenye nyumba ya udongo anakuzidi mara mia wewe unaepanga gorofa zima. jitambue

      Delete
  2. SIFIA KUJENGA NA SI KUPANGA

    ReplyDelete
  3. Upuuzi mtupu. Mie nilidhani kajenga au kanunua

    ReplyDelete
  4. Jitahidi ujenge na siyo kupanga, Nyumba kama siyo yako hata iwe nzuri kiasi gani ,vitu vya gharama ni bure jenga yako lol

    ReplyDelete

Top Post Ad