Mke wa LOWASSA Aondolewa Mkutanoni Simiyu na Kupitishwa Mlango wa Nyuma Kisa Hichi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mke wa Lowassa Mama Regina Lowassa
MGOGORO wa vyama viwili vya siasa CUF na CHADEMA ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, juzi ulichukua sura mpya.

Hali hiyo inatokana na  mgombea mmoja wa ubunge wa jimbo hilo kupitia CUF, Martine Makondo na wafuasi wake, kuvamia uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa CHADEMA, Martine Magire ambapo mgeni alikuwa Mama Regina Lowassa (mke wa Edward Lowassa).

Mama Lowassa alishindwa kuzindua kampeni hizo kutokana na vurugu kubwa zilizotokea. Awali mkutano ulikuwa ufanyike kwenye Uwanja wa Michezo uliopo katika Sekondari ya Lagangabilili.

Dalili za vurugu zilianza kuonekana mapema baada ya wafuasi wa CHADEMA kudai kuwa, mgombea wa CUF alikuwa amekwenda kwenye mkutano huo na kundi la vijana ili kuvuruga mkutano.

Baada ya Mama Lowassa kuwasili eneo la mkutano akiwa na Naibu Katibu Mkuu Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa (BAWACHA),Kunti Yusuph, mgombea wa CUF aliwasili eneo hilo akiwa amebebwa na wafuasi wake wakidai mgombea wao amehujumiwa na mgombeawa CHADEMA na kusababisha jina lake likatwe na Kamati Kuu.

Wafuasi wa CUF walimpandisha mgombea wao (Makondo), jukwaani ndipo  vikaanza kutokea vijembe kati yao na wafuasi wa CHADEMA wakiimba, kupiga kelele za kuwataja wagombea wao.

Hali hiyo iliwashangaza viongozi wa CHADEMA na mgeni rasmi (Mama Lowassa) kwa dakika 15 ndipo walinzi wa chama hicho wakamwondoa eneo hilo wakihofia usalama wake katika mkutano huo.

Baada ya Mama Lowassa kuondolewa jukwaani, kupanda gari yake na kuondoka eneo la mkutano, Yusuph alianza kuwatuliza wafuasi wa vyama hivyo bila mafanikio akaamua kuwatuhumu wananchi, lakini wafuasi walimzomea wakitaka Makondo arudishwe.

"Tatizo tunafanya siasa kwa ushabiki na matokeo yake ndiyo haya, mimi sikuja kunadi mahindi kwenye mnada, nimekuja kumwombea kura mgombea urais wa UKAWA (Edward Lowassa), ubunge na udiwani mtajuana wenyewe Oktoba 25, mwaka huu," alisema.

Hata hivyo, Yusuph alishindwa kutuliza vurugu hizo na kulazimika kuondoka eneo hilo chini ya ulinzi wa vijana wa CHADEMA na kuwaacha viongozi wa mkoa, wilaya waendelee na mkutano lakini hata baada ya kuondoka, mkutano huo haukuendelea.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gemin Mushy, alisema askari wake walitumia busara kutomtoa mgombea wa CUF kutokana na mazingira kutokuruhusu kumkamata.

Chanzo cha mgogoro huo ni Makondo ambaye awali alikuwa CHADEMA, kutimkia CUF baada ya jina lake kukatwa ingawa alishinda kwenye kura za maoni na aliyeshinda nafasi ya pili Magire kupewa nafasi hiyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mweh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!"Tatizo tunafanya siasa kwa ushabiki na matokeo yake ndiyo haya, mimi sikuja kunadi mahindi kwenye mnada, nimekuja kumwombea kura mgombea urais wa UKAWA (Edward Lowassa), ubunge na udiwani mtajuana wenyewe Oktoba 25, mwaka huu,"

    akili kumkichwa sasa

    ReplyDelete
  2. Semeni UKAWA na hapo CCM wanahusika nyie sio wa kupewa nchi ni longolongo na matusi mmejaliwa mwaanza jitafuna wenyewe Mbatia sasa mguu mmoja kaburini na mwingine duniani anasubiria hukumu ya wana NCCR Majeruhi kila mahali mihemuko tupu hapa Magufuli anamalizia kwa kusukuma kwa kidole kazi kwisha asubuhi na mapema ntakemsitake

    ReplyDelete
  3. Hapa goli la mkono la nini hawa UKAWA goli nane kwa sifuri wamesha bugia maana yake wemechanganyikiwa wanahangaika japo wapate goli la kufutia machozi ktk dakika za lala salama

    ReplyDelete
  4. Usitake-ncheke!!

    ReplyDelete
  5. Regina U first lady utakutoa roho tulia kama mama Magufuli wanaokutuma hawakutakii mema siasa za bongo ni ngumu utatolewa kafara

    ReplyDelete
  6. Kazi ya ukawa ni matusi na kusibgizia mamluki wa ccm hao wametumwa kweli mtaisoma namber ukawa

    ReplyDelete

Top Post Ad