UVCCM yamshangaa Sumaye kumpigia debe Lowassa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema anamshangaa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kusaidia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa.

Amesema uamuzi huo wa Sumaye ni sawa na pwagu kumfanyia kampeni pwaguzi. Shaka alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na madiwani jimbo la Mtwara Vijijini wakati akimnadi mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM, Hawa Ghasia.

Mkutano huo wa kampeni ulifanyika katika kijiji cha Mo Pacha Nne mkoani hapa.

Alisema ni kituko kwa viongozi hao, ambao waliwahi kuwa viongozi wa juu wa serikali ya CCM na kushindwa kuleta ufanisi na matokeo chanya, sasa wakiwa Chadema kughilibu wananchi wakidai wana ubavu wa kuleta mabadiliko na maendeleo.

“Sumaye anapomfanyia kampeni Lowassa awe Rais ni sawa na pwagu kumfanyia kampeni pwaguzi, hawajui wafanyalo, hawatambui kama majina yao hayaheshimiki mbele ya jamii, walipewa nafasi za juu wakashindwa kuisukuma nchi kimaendeleo,” alisema Shaka.

Alisema Sumaye akiwa Waziri Mkuu wa Serikali chini ya awamu ya tatu ya Rais Benjamni Mkapa, usimamizi wake alisababisha halmashauri nyingi za wilaya nchini kupata hati chafu kwa mujibu wa ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Aidha, Shaka alifichua siri ya jina la Lowassa kukatwa na vikao vya CCM katika mbio za urais, huku akisema halikuwa jambo la bahati mbaya.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. katibu mkuu wa uvccm anamshangaa mhe.sumaye kumpigia kampeni rais mtarajiwa wa awamu ya tano mheshimiwa edward lowassa.hiki ni kituko.sijui kama ubongo wa huyu katibu upo sawa.hamshangai mgombea urais wa ccm anapomshangaa bosi wake anayemaliza muda huku akiwa na serikali legelege isiyojali shida na malalamiko ya raia,hamshangai warioba aliyevalishwa magwanda ya ccm[ambayo hajawahi kuyavaa tangu 1995] kuwapigia kampeni ccm,hamshangai yusuph makamba anayemnadi mheshimiwa lowassa bila kujitambua,hamshangai januari makamba aliyetoa rushwa ya million 15 pale national stadium akisema ni zawadi ya ccm watazamaji waingie bure mpirani pambano la tanzania na nigeria na wale wale walioingia kwa kulipiwa na ccm kama rushwa waliingia huku wakiimba kwa nguvu na kibwagizo kupokelewa na uwanja mzima LOWASSA RAIS,LOWASSA RAIS,LOWASSA RAIS,PEOPLES POWER,PEOPLES POWER.mwisho hajishangai yeye mwenyewe shoka kumpigia kampeni mgombea urais wa ccm aliyekwisha poteza dira na kukata tamaa anayesema kuwa yeye sasa ni movement for change ya chadema na anawaomba wana ukawa wampigie kura kwa wingi! kweli shoka kageuka kishoka [wale wa tanesco]

    ReplyDelete
  2. huna loloteeeeeeeee kafie mbele na wewe hapo unaongea pumba

    ReplyDelete
  3. mbele siwezi kufia,kwa nini unanitukana wewe mwana ccm,usinionee twende kwenye hoja.kama una hamu ya matusi nakuomba ukae kimya usikilize muziki mnene wa lowassa na kama hujisikii bado kulainika basi jaza maji kwenye kopo uende msalani,hiyo ni haja kubwa iliyokua inakusumbua.ukitoka msalani akili yako ya ukicheche itakuwa imefunguka na,inshallah, utabadirika na sasa utamkubali mheshimiwa lowassa kua ndie rais wetu ajaye.imba;tuna imani na lowassa,oya,oya,oya.

    ReplyDelete
  4. EENDELENI KUSHANGAAAA MAGUFURI, NAE PIA ASHANGAAA, CCM NAYO INASHAANGAAA,SERIKARI NAYO INASHANGAAA KWELI NIAMINI MNARA WA BABELI

    ReplyDelete

Top Post Ad