CCM Walia na Picha za Mikutano ya Lowassa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Teknolojia mpya ya habari na mawasiliano inamchango mkubwa sana kwenye uchaguzi wa mwaka huu, bila shaka imeongeza chachu ya ushindani kutokana jinsi ambavyo habari zinasambaa kwa muda mfupi ukilinganisha na chaguzi zilizopita.

Hata hivyo, teknolojia hii imeibua wasiwasi mwingine kuwa huenda ikawa inatumika katika kufanya udanganyifu kwa kuchezea (manipulate) picha zinazoonekana kuwa za mikutano ya baadhi ya wagombea.

Dr. Emmanuel Nchimbi, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM ameeleza kwa nyakati tofauti kuwa picha zinazoonekana za mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa hazina uhalisia bali zimehaririwa ili kuonekana kuwa alikuwa na watu wengi kwenye mikutano yake.

Baadhi ya makada wa CCM kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakieleza kuwa picha inayosambaa ikionesha mafuriko ya Lowassa hivi karibuni jijini Arusha sio ya kweli bali ni umati wa watu katika nchi moja ya Afrika Magharibi.

Huu ni muendelezo wa tuhuma za CCM dhidi ya Chadema kuhusu picha hizo kwani Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete aliwaeleza wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni zake katika uwanja wa Jangwani, Dar es Salaam, kuwa wasitishwe na picha za Chadema kwa kuwa zimehaririwa na sio kweli.

“Wamechukua picha nyingine za mikutano ya Dk. Slaa, wanaunganisha, waambieni waje waone picha halisi,” alisema.

Hata hivyo, Chadema na Ukawa kwa ujumla walimjibu mwenyekiti huyo wa CCM katika siku ya uzinduzi wa kampeni zao uliohudhuriwa na maelfu ya watu kwa kumtaka aione picha halisi ili aamini kuwa hakuna uhariri katika picha anazoziona.

Je, ni kweli picha za Chadema zinahaririwa? Swali hilo tunawaachia watazamani wa mikutano hiyo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HA HA HA HA HA HA AFRICA MAGHARIBI? DAH NIMECHEKA SUBURINI 25/OCT NAONA NDIO MTAAMINI, CCM MWAKA HUUU HAKUNA RANGI HAMTA ONA TUMESHAAMUA KUWA DELETE MWAKA HUUU NENO CCM DUNIANI HATUTAKI KULISIKIA TENAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. Peoplesssssssss

    ReplyDelete
  3. Wingi wa unawatisha CCM

    ReplyDelete
  4. yanatapatapa, mabadilikooooooooooooooo!!!!! lowasaaaaaaaaaaaaaa!!!! lowasaaaaaaaaaaaa!!!! mabadilikooooooooooooooooo!!

    ReplyDelete
  5. CCM HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  6. wingi wa watu ingekua ndio kupiga kuraa basi ingeku raha sanaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na matusi na vijembe Na wasanii maarufu ingekuwa kura mbona raha

      Delete

Top Post Ad