Haji Duni agundua janja ya CCM,waliopangwa kuchakachua matokeo watajwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Haji Duni amesema kuwa wamegundua njama iliyopangwa na Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Tume ya uchaguzi kwamba kura zikitoka kwenye vituo zipite kwenye mtandao na kuziiba kwa kutumia wataalamu wao wa TEHAMA.

Ameyasema hayo mapema leo wakati wa kufunga kampeni kwa vyama vinavyounda umoja huo zilizofanyika katika viwanja vya jangwani jijini Dar es Salaam

Duni  amesema kuwa CCM imetayarisha wataalam wawili ambao watafanya kazi hiyo na kwamba UKAWA watajitahidi kuweka kumbukumbu iliyosahihi ya matokeo ya kura zao zote ili kuepusha wizi unaotaka kufanywa.

Ameongeza kuwa kila wakala lazima apatiwe nyaraka ya matokeo ya kura iliyotiwa saini,

Aliwataja wataalam hao kuwa ni Mr Mkanyanga na Sesy Francis ambao ndio wamekabidhiwa kuiba kura katika kituo cha Kurasini karibu na makao makuu ya uhamiaji.

“Wakileta mchezo tutawaambia wananchi wakakizunguke alafu tutaona kama hodari ni Rais Kikwete au wananchi …..Kikwete umeambiwa ukabidhi nchi kama ulivyopewa kwa amani na akuna Jeshi linaloweza kupiagana na umma,”amesema Duni.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad