Hali si shwari Tarime, Sita wakatwa mapanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu sita wamejeruhuiwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao  Wilayani Tarime mkoani Mara akiwemo mwandishi wa habari wa Sahara Media, Geoge Nteminyanda (49) usiku wa kuamkia leo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi katika wodi namba tatu na namba nane walikolazwa, majeruhi hao wamesema kuwa walishambuliwa na wafuasi wa vyama vya Chadema na CCM ambao walikuwa katika makundi makundi kati ya saa mbili na saa nne usiku.

Nteminyanda ambaye ni mkazi wa Kisesa  Mwanza amesema kuwa aliitwa na mgombea ubunge wa CCM, Michael Kembaki na kufikia katika hoteli  ya CMG ambapo kulikuwa na kikao cha chama hicho lakini alianza kuhojiwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho. Lakini licha ya kutoa vitambulisho vya kazi wafuasi hao walianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga mwilini na kuanguka chini. Hata hivyo watu hao waliendelea kumkanyaga hadi akapoteza fahamu.

Wasamaria wema walimchukua na kumpeleka hospitalini ambapo alipewa kitanda namba tatu cha wodi namba tatu.

“Waliokuwa wakinishambulia walikuwa vijana wengi kutokana na kunikabiri vibaya sikuwatambua kwa haraka lakini wakiwekwa kwenye mstari wa utambuzi nitawatambua” amesema Nteminyanda.

Wengine waliojeruhiwa ni Waiboga warioba (37) aliyekatwa kichwa na sikio la kulia,Busiro Rhobi (28) mkazi wa Nyamongo aliyekuwa na gari lake binafsi, Daniel Mathew (18) mkazi wa Goribe Wilayani Rorya anayedaiwa kupigwa risasi kichwani upande wa kulia na mgombea udiwani wa kata ya Ikoma  Laurence Andriano (CCM).

Wengine ni Wambura Marai (38) aliyeopolewa kutoka kwenye gari lake baada ya kutokea ubishani kati yake na wafuasi wa CHADEMA kuwa mshindi urais atakuwa John Pombe Magufuli.

Rose Hosea muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Tarime amesema kuwa wakati wanapokelewa hali yao ilikuwa mbaya zaidi lakini kutokana na juhudi za timu ya wauguzi wa zamu walitoa huduma za haraka ikiwa ni pamoja na kuwashona majeraha yao huku wakiwapa dawa za maumivu.

“Hali yao inaendelea vizuri kwa sasa tofauti na ilivyokuwa jana” amesema Hosea.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad