LUNGI Amlipua Agness Masogange..Adai Ana Umbo Zuri Lakini Ameshindwa Kulitumia Kiasi cha Kumtelekeza Mtoto Wake na Hata Gari Zuri Hana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSANII wa siku nyingi kwenye anga la filamu Bongo, Lungi Maulanga amemlipua Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kwamba hajui kutumia umbo lake vizuri ndiyo maana amemtelekeza mwanaye.Akipiga stori na Ijumaa, Lungi alidai Masogange amemwacha mwanaye kwa shangazi yake huku malezi yake yakiwa duni wakati yeye akijiachia kimjini.

Masogange ananichefua kwa kuwa amemtelekeza mwanaye, mimi nina watoto watatu na ninahakikisha wanasoma shule nzuri sasa yeye huyo mtoto mmoja tu anamshinda, anamsomesha shule za kayumba, inakuja kweli hiyo?
“Halafu Mungu amemjalia kuwa na umbo zuri, sasa angekuwa analitumia vizuri angeshindwa kumlea mwanaye katika mazingira mazuri mpaka akamwache kwa shangazi wake. Mbaya zaidi hata gari zuri hana, sasa umbo lake linamsaidia nini?” alisema Lungi.

Baada ya paparazi wetu kumsomea mashtaka Masogange, mrembo huyo alisema: “Mwanangu nilimpeleka kwa baba yake, kama ingekuwa nimemwacha kwa marafiki au sehemu nyingine hapo ningeambiwa nimemtelekeza, kuhusu mafanikio yangu siwezi kutangaza kwamba nina hiki au kile.

Gari ni kitu cha kawaida sana, kitu cha maana ni nyumba sasa siwezi kuanika mambo yangu. Kuhusu umbo zuri huyo dada alitaka nijiuze? Siwezi kufanya biashara chafu mimi.”

By Gladness Mallya na Hamida Hassan/Globla Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad