Mbowe Afichua Njama Za CCM Kuiba Kura Usiku wa Tarehe 24

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema wamegundua njama za kuiba kura zitakazofanywa na CCM usiku wa tarehe 24 kwa kupita mitaani na kugawa fedha za kura feki.

Mbowe alitoa  kauli  hiyo  jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe vilivyopo jijini Mbeya.

Alisema ili kudhibiti hali hiyo, siku hiyo Ukawa watafanya doria usiku kucha ili kuhakikisha hakuna fedha zinazogawiwa wala kura feki zitakazosambazwa.

Nia ya Ukawa ya kupigania Katiba ya wananchi iko pale pale kwani Serikali ya awamu ya tano itaipigania kadri itakavyowezekana ili kiu ya wananchi juu ya Katiba hiyo ipatikane,” alisema Mbowe.

Alisema pia kwamba, uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa kuwa unahusu maisha ya watu, watoto na utajibu maombi ya Watanzania.

Pamoja na hayo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), siyo huru  na kwamba wanachama wa Chadema watahakikisha wanalinda kura zao.

Kwa miaka 25 tumepiga kelele tukidai tume huru ya uchaguzi lakini kilio chetu hakikusikika kwa sababu CCM inajua tukiwa na tume huru, haiwezi kubaki madarakani.

“Kama tume yetu siyo huru, tuna wajibu wa ziada wa kulinda kura zetu. sheria inasema huturuhusiwi kusimama wala kukaa chini ya mita 200 kutoka kituoni. Kwa hiyo, ukihesabu mita 200 kutoka kituoni, una uhuru wa kuwa eneo hilo,

Jambo hili limezua hofu ndani ya tume, ndani  ya Serikali, ndani ya CCM na kwa Rais Jakaya Kikwete kwa sababu anasema tukishapiga kura, tukalale. Sasa namwambia Rais Kikwete ushauri huo akawape CCM, sisi hatuutaki,” alisema Mbowe.

Alisema pia kwamba, wanachama wa Chadema na wapenzi wao, hawatafanya fujo bali watakuwa na ujasiri wa kupiga na kulinda kura zao kwa sababu hakuna anayeweza kuzuia mpango wa Mungu kwa kutumia askari au nguvu.

Source:Mpekuzi blog
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad