PROF Lipumba Aibuka...Aishukia ZEC Kufuta Uchaguzi Zanzibar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyikiti Mstaafu wa Chama cha Wananchi Cuf, Prof Ibrahim Lipumba amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha amekiuka sheria kwa  kusitisha utangazaji wa matokeo kwani inaweza kuleta mgogoro wa kisiasa.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Azam Tv, Prof Lipumba amesema mwenyekiti wa ZEC alipaswa kuita majaji na wajumbe wa tume na kujadiliana na kuwatangaza walioshinda na lisichukuliwe kisiasa.

“Huwezi kufuta matokeo ya urais Zanzibar halafu useme uchaguzi wa Tanzania ni halali,”amesema Lipumba

Amesema katika katiba ya Zanzibar Ibara 28 (2) inasema rais atachia madaraka yake baada ya kumaliza miaka mitano na kuongeza kuwa mwenyekiti wa ZEC amedai kuwa kuhairishwa kwa matokeo ya urais kumesababishwa na kuwa na wapigakura wengi  zaidi katika vituo kuliko wale walioandikishwa.

“Suala hilo walipaswa waulizwe wasimamizi na mawakala na kulalamika siku ile ya uchaguzi,”.alisema Lipumba
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad