Tanzania Tumefika Pabaya..Kada wa CCM Amwagiwa Tindikali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tarime. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Chadema kata ya Sirari na kuhamia chama cha CCM, Weng’ari Mang’era (26) amemwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati wakimpokea mgombea ubunge wa Tarime Vijijini(CCM), Christopher Kangoye katika uwanja wa Tarafa Sirari Wilayani Tarime.

Shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe litajwe ameeleza” Mbunge Kangoye alikuwa anakwenda kwenye mkutano Uwanja wa Tarafa wakati tuko barabarani watu wakafika na kumjeruhi kwa kumwagia tindikali,’amesema.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Lazaro Mambosasa amesema polisi wanafuatilia kujua waliohusika na tukio hilo.
Wakati hilo likitokea, Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Athuman Akalama alisimamisha kampeni kwa wagombea zilizokuwa zinaendelea Nyamongo baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya CCM na Chadema.

Leo asubuhi mgombea Udiwani Kata ya Matongo-Nyamongo(CCM), Daud Itembe akiwa kwenye harakati zake za kuhitimisha kampeni zake zilizokuwa zifanyike maeneo ya stendi Nyamongo lakini kukaibuka vurugu kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad