UTABIRI wa Mgombea Urais TZ Kufariki Kabla ya Oktoba 25 Umetimia?! Haya Ndio Majibu ya MAALIM Hussein!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MTABIRI maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein, amesema utabiri wake alioutoa mwaka 2014 kwamba mgombea urais mmoja atafariki dunia ghafla kabla ya uchaguzi, umetimia baada ya kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila na kuwaacha salama wagombea Edward Lowassa na Dk. John Magufuli.
Maalim Hassan aliyasema hayo alipozungumza na gazeti hili juzi ambapo alisisitiza kuwa utabiri wake alioutoa Desemba 28, 2014 katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake, haukumlenga mtu.

Mchungaji Mtikila ambaye alikuwa akigombea urais kupitia Democratic Party (DP) kabla ya kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), alifariki dunia Oktoba 4, 2015 kwa ajali ya gari kijijini Msolwa, Chalinze, mkoani Pwani akitokea Njombe.
“Nilipoutoa utabiri ule mengi yalisema na watu wakawataja wagombea fulani, lakini niliwaambia kwamba utabiri haulengi mtu na sasa umempata Mchungaji Mtikila.
“Mtikila alikuwa mgombea urais, alichukua fomu na watu wakaona akiwa na mkoba kama wa wagombea wenzake, akakataliwa na tume lakini akakata rufaa… angeweza pia kushinda rufaa yake,” alisema Maalim Hassan.
Aliongeza kuwa, mara baada ya utabiri wake alipigiwa simu na makada wa vyama viwili – Chama cha Mapinduzi (CCM) waliodai kuwa mgombea wao Dk. Magufuli haumhusu na wale wa Chadema nao wakasema mgombea wao, Lowassa hawezi kuchuliwa hivyo – akawajibu wote kwamba utabiri wake haumlengi mtu.
“Niwahakikishie wananchi kwamba, kinyota wagombea wote wa urais waliobaki sasa wako salama na watashiriki kuchagua viongozi Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Maalim Hassan.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huna mpango wewe yote Kazi ya mungu Na laana kwa kumtukana Lowassa
    Bado wengine Hasa Makongoro Na Nape Na Makonda
    Kigoda Na Celina wanawasubiri Akhera

    ReplyDelete
  2. Acha uongo wewe shehe kibaka niloge Mimi. Na taja jina langu hapa wapi naishi
    Yote Kazi ya mungu tapeli mkubwa wewe
    Kama baba yako

    ReplyDelete
  3. Hahahahahaha wa tanzania si wawezi kwa matusi

    ReplyDelete
  4. Maalim nani huyo Hussein zamani tulikuwa tunampa makonzi sana Kinondoni/Bangladesh wakati wanakaa kwa baba yao mkubwa yeye na ndugu yake wa kuitwa Hassan nashangaaga sana nikisikia eti sasa amekuwa mtabiri kwa kisomo kipi?Wajinga ndio waliwao

    ReplyDelete
  5. sio kweli Mchungaji Christopher Mtikila hakuwa mgombea ui rais mwaka huu alikatwa mapema sana

    wacha kutafuta sifa za bure hapa tapeli mkubwa wewe

    ReplyDelete
  6. Mungu pekee ndio mjuzi na mwenye nguvu. yeye akisema kua ndio jambo kua ndio linakua. nakumbuka ulitaja mamba wako ambao ulisema nyota ndio zinasema miongoni mwao mmoja ndio atakua raisi. Uliwataja kabisaaaa - Makamba, Membe, Migiro, Jaji Augostino na wengine wote ukawaita kenge tu na ni wasindikizaji. Wote wale chaliiiiiiiiii amewekwa magufuli na yeye anapigwa chali na Mzee Lowassa tarehe 25.
    Kiukweli utabiri wenu ulilenga kumtisha lowassa kwa kua mnatumiwa kisiasa. Mzee bado anasonga na kwa uwezo wake Mungu yeye ndio atakua raisi.

    ReplyDelete

Top Post Ad