Wasomi Mmemsikia Edward Lowassa? Mikopo ya Elimu ya Juu Kupatiwa JIbu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kile kilio cha siku nyingi cha maumivu ya mkopo wa elimu ya juu kinakaribia kupatiwa jibu. Mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa ameahidi kuwasamehe wale wote waliokopeshwa na kodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Lowassa anamaanisha kuwa wanaodaiwa hawatalipa tena na itakuwa ni kama wamesomeshwa bure tu na Serikali yao.

Wakati huohuo, Lowassa anaendelea kusisitiza kuwa elimu ya chuo kikuu itakuwa bure. Wasomi wa wakati wa nyuma na wale wa sasa, mnataka nini tena? Lowassa, kutokana na ahadi zake za kiuchaguzi, anatamani kuona elimu inakuwa bure na hata wale waliokopeshwa wakijisikia kuwa wamesoma bure. Lengo kuu ni kutoa elimu ya bure na bora kwa maendeleo ya Tanzania yetu.

Mtampa kura wasomi wa Tanzania? Wale waliolipa hadi kumaliza mkopo, Serikali itawarudishia fedha zao? Tutege masikio tena kumsikia Lowassa atalisemeaje hili.m
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante kwa kuwa na wazo la kufuta mikopo maana hata mimi nina mkopo,japo sasa hivi nafanya shughuli zangu mwenyewe na sifikirii kuajiriwa,naajiri.Ila bahati mbaya hutamshinda Magufuli kwa maana hiyo ahadi imeota mbawa tayari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Migufu hafui dafu kwa Lowassa.waweke meza moja magufuli ameshalewa.lowassa mtulivu hakurupuki atafikiri kwanza kabla ya kufanya lolote.

      Delete
  2. Pia atuhakikishie kwamba yeye fisadi papa atazirudisha fedha zetu zote alizotuibia waTZ, pale alipotudanganya kwamba eti amekwenda kununua mvua.........

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chenge, tibaijuka, jk , na majizi yote ya CCM watalipa lini

      Delete
    2. swali zuri sana, hao wote ulowataja pamoja na Lowasa na wengine ambao hukuwataja, wanamsubiri Muheshimiwa sana JPJ Magufuli akiapishwa tu, atawafungulia mahakama yao 'spesho' ili wafungwe haraka baada ya kufilisiwa....UPO HAPO??

      Delete
    3. Majizi yote na magufuli yupo naye
      Kinana , mkapa

      Delete
    4. Magufuli ni pombe. Ni mtenda kazi. lakini kimataifa hafui dafu. Jinsi zungumza yake haipo sawa. Ukishindwa zungumza lugha umeshajisikia chini. Hutaweza kusimama kidete na wenye lugha yao. Utaona aibu na kunywea. Mnapomchagua Raisi mtu kama magufuli, Asiyejua lugha, kwanza mnajushusha kama nchi kielimu. Analugha ya kuombea maji. Uraisi ni kuweza kuzungumza na mataifa yanayoiangalia Tanzania kwa jicho kali. Tumefikia hapa tulipo sababu viongozi wetu wengi wa ngazi za juu hawaimudu lugha sawasawa.Wanajikuta wanakaa kimya, kucheka, au kukubaliana na jambo ambalo hajalielewa sawa. Wengi viongozi wa juu wa CCM wanatatizo hili. Hawajui kuzungumza lugha. Wanapewa na kuisani mikataba bila kukijua kiundani walichokisaini.Anapewa kipesa benki kashiba. Na wasomi karibu wote waliochaguliwa kwa kipindi cha ndugu Kikwete wameiangusha nchi sababu ya rushwa na kuachiwa huru na Raisi mwenyewe. Unawategemea watu kutendea haki Wananchi bila mwenyewe kujua linachofanyika. Kwa miaka kumi Ikulu imejaa watu kama hawa waliotawala nchi kindugu kutokana na kiongozi dhaifu na kuwaachia wafanye watakalo. Usipokuwa mjuzi wewe kama kiongozi matokeo ni haya. Magufuli atakuwa kama Kikwete au zaidi. Hataweza kuwafanyia kazi hao mliowataja juu. Hana ubavu wa kuwadhibiti. Wanampigia debe leo na itambidi arudishe fadhila kwao wote pamoja na Wasanii wanaompigia debe.haya ni madeni ambayo itabidi ayalipe. Hakuna mtu hata mmoja CCM mwenye nia njema na Watanzania wa kawaida.Wote wanatetea maslahi yao waliyojijengea enzi za Kikwete.

      Delete

Top Post Ad