Dr. Slaa: Magufuli Haogopi Kupoteza Kura Kwa Kukemea Ufisadi na Kusema Atawafunga Wala Rushwa....Awalinganisha Lowassa na Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtangazaji anatambulisha mada. Ni yule yule Kamonte aliyemhoji mara mbili zilizopita.

Dr. Slaa: Nitaendelea kupigia kelele mambo yanayohusu taifa langu

Dr. Slaa: Uchaguzi huu ni wa kipekee. Watanzania wanataka mabadiliko. Umma haujatafsiri maana ya mabadiliko

Dr. Slaa: Dhana ya mabadiliko haijaelewa vyema. Dhana hii si mpya. Ilisemwa hata na Hayati Mwalimu Nyerere

Dr. Slaa: Mabadiliko yana sura mbili. Yapo ya kutoka pazuri kwenda kubaya na ile ya kutoka kubaya kwenda kuzuri. Anatoa mfano wa Dikteta Benito Mussolin wa Italia

Dr. Slaa: Ninahisi tafsiri ya mabadiliko haijaeleweka. Hata wasomi hawaelewi. Kwa upande wa wenzetu wapinzani wanachukua mifano ya hata Marekani ambapo Obama alikuwa na sifa..

Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna kauli za kutishia kuingia barabarani

Dr. Slaa: Wapo wenye tamaa ya kwenda Ikulu. Hiyo si ambition ya uongozi. Ambition inaambatana na maandalizi

Dr. Slaa: Kumchagua Rais si suala dogo. Tutavumilia kwa miaka mitano

Dr. Slaa: Amani inapaswa kuwa ajenda kuu kwakuwa ni zao la demokrasia.

Dr. Slaa: Naungana na Jaji Warioba kuwa rushwa ilikuwa inatisha. Serikali za Mitaa hupewa asilimia 23 za bajeti. Asilimia 75 ya 23 hupotea kwa rushwa. Kuna grand na petty corruption. Rushwa ndogo huumiza kuliko kubwa kwakuwa zinagusa watu wanyonge.

Dr. Slaa: Katika kampeni za mwaka huu,chama changu CHADEMA kimeacha ajenda ya rushwa. Hata nyimbo za hamasa za kupinga rushwa hazisikiki. ACT ni kama wanairithi CHADEMA kwenye ajenda ya rushwa. Nampongeza Zitto na chama chake. Yuko committed

Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna kauli za kutishia kuingia barabarani

Dr. Slaa: Dr. Magufuli anasisitiza kuwa anapiga vita rushwa. Sijaona jambo hilo kwa CHADEMA. Ukiwa mchafu huwezi kukemea. Dr. Magufuli anasema ataanzisha Mahakama Maalum za rushwa na ukimtazama anaaminika. Dr. Magufuli sijawahi kusema ni msafi. Lakini ana nafuu kati ya wagombea nane

Dr. Slaa: Tulimpinga Rais Kikwete mwaka 2010 kuwanyanyua Mramba,Chenge na Lowassa. Magufuli haogopi kupoteza kura kwa kukemea ufisadi na kusema atawafunga wala rushwa. Magufuli ni jasiri

Dr. Slaa: Kuna michakato inafanyika kama kuwaleta na malori na mabasi. Chama changu kilikuwa hakibebi watu. Lakini kilibeba kwenye mkutano wa Jangwani.

Dr. Slaa: Baada ya kusikiliza na kuona mikutano,kwanza tujiulize tunataka Rais wa aina gani. Mwenye vigezo vya kupambana na rushwa, Magufuli anafaa. Rais hawezi kuongea kwa dakika kumi, nani atakuwa Rais? Ni akina Sumaye?

Dr. Slaa: Tanzania ni mama yetu. Tukichezea amani ya Tanzania,sote tutaathirika. Nawaomba NEC wasimamie sheria. Watanzania tusimamie amani yetu.

MSIKILIZE HAPA KWENYE HII VIDEO:
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

25 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lowassa hawezi kukemea rushwa wala ufisadi kwa kuwa ana kashfa ya ufisadi na mtoa rushwa namba moja.MUNGU IBARIKI TANZANIA,TUPE UELEWA WA KUMTAMBUA NANI ATAENDELEZA AMANI HII.

    ReplyDelete
  2. Pumbavu hili yuda wewe
    First Lady umekuponza
    Umetusaliti hatukupendi hadi akhera wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole,CCM tunampenda,na ndio Chama kubwa.
      Tukutane kwenye foleni 25/10/2015

      Delete
    2. CCM mnampenda kwa sababu mnapenda mgongo

      Delete
  3. Magufuli ni jembe hili halina kipingamizi hata wapinzani wanatambua kuwa mziki wa magufuli ni mkubwa ila wanajifariji tu kwa kuwa hawawezi kuishia njian wanajikaza mpaka cku ya mwisho lkn ukweli unafahamika kuwa magufuli ndo Rais hata malaika wanajua kwa kuwa ni chaguo la Mungu. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI MAGUFULI. AMEN!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. UMECHELEWA WALA HUNA JIPYA, MSIMAMO NI LOWASAAAAA!

    ReplyDelete
  5. MPUMBAVU MMBWA WEE.TULIPOKUA,NA TUNAPOENDELEA KUSEMA WEWE SLAA NI MSALITI MKUBWA WA MABADIRIKO HAPA TANZANIA,HATUKUKOSEA NA HATUJAKOSEA.HAKUNA ADUI MKUBWA KAMA WEWE,YAANI AFADHALI YA MACHIZI WENZIO NAPE NA JANUARI.NAWAPA AFADHALI HII KWA SABABU NI WAO NA UHAI WA CCM.WEWE SIO,BAADA YA KUNUNULIWA NA CCM KUPITIA MIKONO YA MARANGIRANGI MWAKYEMBE UMEHARIBIKIWA KABISA.YAANI KAULI ZAKO KAMA VILE UNAZITOA MATAKONI.YAANI UNAKERA MNO.SASA NAZUNGUMZIA ULICHOKISEMA.AWALI YA YOTE UMEJIFAFANUA NA KUJIPAMBANUA KWAMBA WEWE SI MPINZANI TENABALI NI CCM. .KWENYE JIBU LAKO LA TANO LA MWANDISHI ALIYEKUHOJI UNASEMA NAKUNUKUU "WENZETU WA UPINZANI BADO HAWAJAIELEWA DHANA YA MABADIRIKO" MWISHO WA KUNUKUU.NAWAULIZENI WATANZANIA WOOOTE,WOTE KABISA TUNAOSUBIRIA UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU,KAZI TUTAKATOIMALIZA KWA AMANI NA UTULIVU SIKU YA KUPIGA KURA JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015 TUTAKAPOMPIGIA KURA ZETU ZOTE ZA VEMA [TICK]MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA NA KUHAKIKISHA ANASHINDA KWA KURA NYIGI MNO NA KUCHUKUA DOLA,JEE BADO YUPO MMOJA WENU ANA SHAKA KWAMBA SLAA NI MWANACHAMA WA CCM? NA TENA AMEONGEZWA NA KIKWETE KUWA MJUMBE WA 33 WA ILE INATOITWA 'KAMATI YA USHINDI YA CCM' KESHA JIPAMBANUA KWAMBA YEYE SI MPINZANI TENA.MIMI NASEMA HIVI SIKU LOWASSA ATAKAYOTANGAZWA MSHINDI LABDA ATOROKE NCHI.HUYU KIKWETE ANAYEMCHOCHEA ATAKUA ANARUDI MJINI KAMA RAIA WA KAWAIDA NA MDOMO KAFUNGA.WAKATI HUO ANGA ZA TANZANIA ZITAKUWA ZIMETAWALIWA NA MWANAUME MMOJA TUU MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA RAIS WA AWAMU YA TANO YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.SLAA UTAJAJIFUNGIA CHOONI KULE MSOGA KWA RAFIKI YAKO JAKAYA MWAKA MZIMA,HAYA WE ZILETE ZA KULETA TUU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SASA NDUGU MATUSI YOTE HAYO YA NINI? SI UONGEE KISTARABU. NA HUYO LOWASSA ASIPOSHINDA SI UTAUWA WATU KWA HASIRI YAKO? POLE SANA NDUGU MAANA NAONA UMKELEKETWA SAAAAANA

      Delete
    2. Anastaili matusi zaidi ya haya
      Lowassa anashinda
      Mwaka huu
      Hakuna kuiba kura CCM
      Mkiiba patakuwa hapatoshi Tanzania

      Delete
    3. Hivi ndivyo wanavyofundishwa wafuasi wa UKAWA,ni matusi,vurugu, hata wakikuta mtu kavaa rangi ya CCM inakuwa shida,halafu unanishawishi nichague Lowasa?KWANGU HAIWEZEKANI! HAPA KAZI TU

      Delete
    4. Tunajibu si mlianza tangu jagwani
      Lile fuso lenu kutuita sisi wapumbavu na malofa
      , wakati ndo loaf anakula makombo ya Mramba wanawake wote duniani

      Delete
  6. Anahitaji maombi huyu mzee !!!

    ReplyDelete
  7. "Anaejua hawezifanya; Anaefanya hajui lolote" kweli hizi ni JUHUDI za WASIOJIWEZA....duuuuuh!!!!

    ReplyDelete
  8. SHIKAMOO C.C.M.

    ReplyDelete
  9. Lowasa huyo huyo alipotajwa pale Mwembe yanga kwamba ni fisadi papa, mlichekelea kwakuwa alikuwa CCM, leo Lowasa huyo huyo yupo chadema akitajwa kama fisadi nyangumi mnatukana!! Inaelekea hata nyinyi wanachama wa chadema mmeridhika na kufurahia chama chenu kuuzwa - hongereni kwa matusi yenu na hongereni kwa kupata mgao wenu......... CCM oyeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  10. yaani nashindwaga kuelewa sijui kwa nini hawa wenzetu huwa wanajazba saana! dah haya sio ya kuandika kabisa unatia huruma. sasa kwa taarifa wote watanzania sio wajinga kama wewe huyo lowasa wako hatopita mimi nakukuhakikisha. mimi nilikuwa chadema lakini kwa sasa no uchaga ndio umetawala kwenaye hicho chama tumewachoka jamani. akili cha kuambiwa changanya na za kwako

    ReplyDelete
  11. HAKUNA MSAMIATI WA LOWASSA KUSHINDWA KWA SABABU TAYARI AMESHASHINDA.KUSHINDWA? LOWASSA KUSHINDWA?TUNAOMBA FUTA HILO AKILINI MWAKO.NEVER,ABADAN,AADAN.

    ReplyDelete
  12. kuongea kistaarabu,wewe hivi upo kweli hapa tanzania?umeshuuhudia au kusikia mvua ya matusi yanayotoka midomoni mwa vinara wapiga debe wa wagombea urais wa ccm , wana ccm-makongoro,nape,msukuma,january,yusuph,mwakyembe,pinda,bulembo,kinana,masaburi,lusinde,shaka -wangapi hao? na orodha ndefu sana sana inaendelea,tumewaorodhesha.tuuenzi wimbo wa marehemu mbaraka mwishehe mwaruka "anza wewe nami namaliza,bora tusielewane vibaya" upo hapo,mpo hapo mliobaki bado ccm? au tuwaimbie tena?ukinirushia hua,nitakujibu kwa kukurushia hua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao wote ulowataja wanafahamika na kazi zao zinajulikana, haya na wewe mwenzetu 'anonymous' kama sisi, ndio nani?? au Da'mbatia?

      Delete
  13. UMEWAKOMESHA CCM,KIMYAAAA.YAMEWAINGIA KISAWA-SAWA.WANAANZA WAO KUKASHFU,KUTUKANA WAKIJIBIWA KOSA.UBONGO WA PANZI!.

    ReplyDelete
  14. Tumesikia kukemea ufisadi miaka 53 nothing happened
    Kukemea na kuongea it's the motto of CCM
    Tumechoka tunataka vitendo
    Lowassa he is the action man without bla bla bla bla bla

    ReplyDelete
    Replies
    1. Katika hiyo miaka 53 huyo lowasa wenu alikuwa wapi?? Alikuwa chama gani?? Alikuwa na cheo gani?? FIKIRI KWANZA KABLA YA KUROPOKA

      Delete
    2. Alikuwa CCM

      Delete
  15. Fisadi no ni jk
    Watu wanashindwa kwenye kura za maoni kwenye chama chenu kugombea ubunge mnawapa ukuu WA wilaya huu ni ufisadi mamboleo
    Kutumia madaraka vibaya
    Lakini atakaa wiki mbili tu Kwani ukawa Hakuna cheo cha mkuu WA wilaya

    ReplyDelete

Top Post Ad