CCM Washikana 'Uchawi' Baada ya Kulipoteza Jimbo La Bunda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BAADHI ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bunda wamemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa, Chacha Gimanwa, kwamba alichangia jimbo la Bunda Mjini kuchukuliwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Vijana hao walitoa tuhuma hizo, juzi wakati wakitembea matembezi ya amani ya kushangilia ushindi wa mgombea urais wa CCM, Dk Jonh Magufuli katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bunda.
 
Katika uchaguzi mkuu uliopita CCM ilipoteza jimbo hilo, baada ya Stephen Wasira aliyekuwa akitetea kiti hicho kushindwa na mgombea wa Chadema, Ester Bulaya.

Hata hivyo Wasira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza alidai kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na hujuma.

Wanachama hao wa CCM wakiwa wamebeba mabango baadhi yao walisikika wakimtaja moja kwa moja Gimanwa kwamba ndiye alisababisha CCM kushindwa katika jimbo hilo na kuomba uongozi wa juu wa chama hicho umchukulie hatua.

Hata hivyo, Gimanwa akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu jana alisema kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote na kwamba kamwe hawezi kukihujumu chama chake.
 
“Hicho ni kikundi cha watu wachache tu wanaotaka kuniharibia jina.Mimi kura yangu ni moja na wapiga kura ni wengi, sasa iweje mimi nisababishe mgombea wa jimbo la Bunda mjini ashindwe?” Alihoji.

 Alisema yeye kama mwenyekiti wa CCM alikuwa akifanya kampeni pia katika jimbo la Bunda vijijini, na siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu alirudi tena Bunda mjini na kuendelea na kampeni.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante mheshimiwa esther bulaya kwa ushindi wako wa kihistoria wa jimbo la bunda.wassira aliifanya bunda mali yake,sasa hivi anaugulia na sijui kama tutamsikia tena kwenye siasa.amekumbana na mwisho wa aibu kubwa.esther mtoto wa kumzaa kamvua nguo babu,anahangaika kutafuta kipande cha kujisetiri.alimfanyia njama chafu esther. kwa mamia.esther wakati wa kampeni kawekwa ndani mara sita,team campaign yake inafika hata mara ishirini.mlikua mkiwatia hasira wananchi,na wamefanya kweli.kwa heri DUBWANA WASSIRA,umekwisha,kwisheni.

    ReplyDelete
  2. mheshimiwa stepen wassira,mjumbe wa kamati kuu ya ccm,waziri wa nchi ofisi ya rais-utawala bora[akiisimamia idara nyeti ya usalama wa taifa],mtunzi wa ilaani ya uchaguzi wa ccm[2015-2020].nilikua najaribu kukugusia tuu wasifa wa stephen wassila katika ccm na serikali.kuangushwa kwa wassira haikuwa rahisi,hakikua kitu kidogo.kuangushwa kwa wassira ni sawasawa na kuangushwa kwa ilani ya uchaguzi ya ccm.ni pigo kubwa sana sana kwa ccm,ni aibu kubwa ya miaka.wakati wa kampeni wassira aliwatumia polisi wa bunda kama mali yake.walimkamata esther bulaya zaidi ya mara kumi,waliyakamata magari yake ya kampeni zaidi ya mara ishirini,waliwakamata timu ya kampeni ya bulaya karibu kila siku ya kampeni.kwa aina hii ya matumizi machafu ya mabavu,maonezi ya wazi,matumizi mabaya ya ofisi wassira anatakiwa ashitakiwe,na wale aliokua akiwatumia wanaweza kuwa mashahidi wazuri sana.AMEANGUKA DIKTETA WA BUNDA.aendelee kulaaniwa huko anakougulia.atafutwe kwa kushtakiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad